Jengo la Ofisi ya Makao Makuu mpya ya Uhamiaji lililoahidiwa na Mhe. John Joseph Pombe Magufuli mapema mwaka jana alipoitembelea Idara hiyo kuzindua Pasipoti za Kielektroniki laanza kujengwa, jengo hilo jipya la ghorofa nane litakuwa Ofisi ya Makao Makuu mpya jijini Dodoma. Jengo hilo la kisasa linajengwa katika viwanja na. 18 na 19 vilivyopo Kitalu A, eneo la NCC, jijini Dodoma.

Jengo hilo lenye thamani ya Shilingi Bilioni kumi litatoa nafasi kwa huduma, na shughuli zote muhimu za kiuhamiaji kufanyika Jijini Dodoma badala ya Kurasini, jijini Dar es Salaam ambako ndiko ilikokuwa Ofisi ya Makao Makuu ya zamani ya Idara hiyo. 

“Kazi itafanywa kwa kasi na waledi, na tunaamini hakuna kikwazo chochote cha kutufanya tushindwe kufikia lengo letu kwa muda wa miezi 18 ya makubaliano na kwa viwango sahihi”, Mhandisi Ujenzi wa SUMA –JKT Ndugu Mahenge alimhakikishia Mkuu wa Kitengo cha Majenzi na Majengo, Mrakibu Mwandamizi Basil Likasi. 

Aidha, Ndugu Simon Mpyanga , Msanifu Majengo toka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam ambao ndio wamepewa jukumu la Mshauri Mwelekezi wa Mradi huu amesema kuwa Taasisi yake ina uwezo wa kutosha kutekeleza jukumu hilo muhimu walilopewa na taifa,. 

Jengo la Makao Makuu mpya ya Uhamiaji ni miongoni mwa ahadi nyingi za Mhe. Magufuli ambazo utekelezaji wake unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.  
 Mtambo wa Kampuni ya SUMA-JKT ukiendelea  na kazi ya kusafisha  eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, jijini Dodoma, ambapo kazi hii ya awali inakwenda sambamba na uwekaji wa Vifaa eneo la Mradi tayari kwa ujenzi . 
 Mkuu wa Kitengo cha Majenzi na Majengo wa Idara ya Uhamiaji (aliyeko katikati), Mrakibu Mwandamizi Basil Likasi akifurahia jambo pamoja na Wahandisi wanasimamia kazi ya kuandaa eneo la Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu mpya ya Idara ya Uhamiaji, eneo la NCC, jijini Dodoma, ambapo kazi hii ya awali inakwenda sambamba na uwekaji wa Vifaa eneo la Mradi tayari kwa ujenzi  
Wahandisi wakijadili jambo wakati wa zoezi la kusafisha  eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, jijini Dodoma, ambapo kazi hii ya awali inakwenda sambamba na uwekaji wa Vifaa eneo la Mradi tayari kwa ujenzi .  Kutoka kushoto ni Mhandisi Umememitambo, Mkaguzi Msaidizi, Kulthum Tamba toka Uhamiaji, katikati ni Mhandisiujenzi , Mahenge kutoka SUMA-JKT, na kulia ni Msanifu Majengo, Simon Mpyanga kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...