Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

KAMATI ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma imeteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo.

Akiongea na wananchi baada ya kuteketeza nguo hizo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwaajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.

Alisema Viongozi wa serikali ya Wilaya walipata taarifa kutoka kwa mkuu wa makazi ya wakimbizi kuna nguo zimeingizwa kambini zinazofanana na sare za jeshi kwaajili ya kuwagawia wakimbizi kama msaada wa nguo.
"Baada ya kupata taarifa wakazifanyia kazi kwa haraka na wakafanikiwa kuzidhibiti na hakuna mkimbizi hata mmoja aliyefanikiwa kupewa"alisema

Anga amewataka wananchi kuacha tabia kutumia nguo zinazofanana na sare za kijeshi kwani ni kosa la kisheria,pia amewataka wale wenye nguo zinazofanana na sare hizo kuzisalimisha katika vyombo vya usalama kama kwenye vituo vya polisi.

"Ni marufuku kuvaa,kusambaza na kuagiza nguo zinazofanana na sare za jeshi ni kosa la kisheria ukipatikana umevaa au kusambaza utachukuliwa hatua kali za kisheria"alisema.Alisema hatua za awali walizochukua mpaka sasa ni wamefungua jalada la uchunguzi,pia wamemkamata mkurugenzi wa shirika lililoungiza hizo,pia wametekeza nguo hizo.

Jumla ya vipande 1947 vya nguo zinazofanana na sare ya jeshi zimeteketezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kiwanja cha mpira cha kawawa kilichopo eneo la Ujiji.
Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikiteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwa ajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.




Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuongoza zoezi la kuteketeza nguo zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa katika makambi ya wakimbizi.
Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akiongoza zoezi la kuteketeza nguo zinazofanana na sare za jeshi zilikamatwa katika makambi ya wakimbizi.
Umati wa wananchi wakishuhudia nguo zinazofanana na sare za kijeshi zikiteketezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika viwanja vya kawawa eneo la ujiji,mkoani Kigoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...