Na Bashir Yakub. 

Wapo watu wanaojua kuwa kuendesha gari kwa mwendo mdogo ndio ustaarabu na ndio jambo zuri linalopendwa sana na sheria. Yeyote mwenye mawazo ya aina hii amekosea sana. Kifungu cha 56 cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya `168 kinakataa dhana hii. 

Kifungu hicho kinasema kuwa “dereva wa gari au teela ambaye bila sababu za msingi ataendesha kwa mwendo mdogo(low speed) ambao utaelekea kuwasababishia watumiaji wengine wa barabara usumbufu au utawasababishia usumbufu, atakuwa ametenda kosa na panapo hatia yake atatakiwa kuadhibiwa kwa kulipa faini”. 

Maneno bila sababu za msingi hapo juu humaanisha kuwa kama itatokea mtu anaendesha kwa mwendo mdogo basi kuwepo na sababu za msingi za kufanya hivyo na hapo ndipo anaweza kukwepa kuingia katika kosa hili. 

Sababu za msingi zaweza kuwa foleni kubwa na hivyo huwezi kuongeza mwendo, unaendesha ndani ya msafara rasmi unaotambulika kisheria, maelekezo ya vibao na alama za usalama za eneo hilo yanakuelekeza kuendesha kwa mwendo huo, ubovu wa barabara ambao haukuruhusu kwenda mwendo mkubwa, barabara imezuiwa na waandamanaji au halaiki(population) nyingine ambayo haikuruhusu kwenda haraka. 

Ubovu wa gari unaweza kuwa sababu ya kutembea taratibu lakini sio sababu ya msingi. Sheria hii inaelekeza gari likiwa bovu kutokuendeshwa barabarani kwa maana ya kuwekwa pembeni ili kulirekebisha au kutafuta namna nyingine. 


KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...