Na Felix Mwagara, MOHA-Kyerwa.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Kyerwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa sokoni mjini humo, leo, Lugola alisema baadhi ya raia wa nchi jirani wamejipenyeza na kujipatia vitambulisho vya taifa ama kwa kuwatumkia wenyeji ama nguvu ya fedha.

“Hii haikubaliki na lazima tuwe makini katika hilo, nimepata taarifa kuhusu watu waliojipatia vitambulisho hivyo ambao hawastahili, kutokana na hilo natoa agizo kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ahakikishe anapitia upya zoezi la kusajili ili aweze kuwabaini ambao walijipatia kwa njia ambazo sio halali,” alisema Lugola.Lugola alisema kuwa, utoaji wa vitambulisho hivyo katika mikoa hiyo unasuasua kwasababu ya umakini unaofanyika katika kusajili waombaji wa vitambulisho.

“Hakuna Mtanzania atakayekosa vitambyulisho vya taifa, kilka mtu anatapa ili mradi tu awe na sifa, na pia mpaka upate lazima upitie mchujo maalumu ili tuhakikishe wewe tunakupa kitambulisho ni Mtanzania halisi au sio.” Alisema Lugola.Aidha, Lugola pia juzi alimuagiza alimpa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika katika mikoa hiyo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa mjini Kyerwa Mkoani Kagera, katika Mkutano uliofanyika katika uwanja wa sokoni mjini humo, leo. Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwasalimia viongozi wa Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, wakati alipokuwa anawasili katika uwanja wa sokoni mjini humo, leo, kwa ajili ya kuzungumza na wananchi. Katika hotuba yake, Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...