Na Amisa Mussa

MADEREVA  wa magari  madogo ya abiria ya Noah na Hiace wilayani Nzega mkoani Tabora wamelalamikia  hatua  zinazochukuliwa  na  Halmashauri  ya  Mji  wa Nzega  kuwakamata  na kuwatoza faini kwa madai  ya kutopakia  na  kushusha  abiria  katika  kituo  mpya  ya mabasi  badala  yake  wanatumia  kituo cha zamani  ambayo  hairuhusiwi  kwa mujibu  wa  namna  walivyosajiri  safari  za  magari  yao.

Wakizungumza na Michuzi Blog ,baadhi ya madereva hao wamelelemikia oparesheni za kamatakamata  zinazodaiwa kufanywa na halmashauri ya mji kwa kile kinachoelezwa kuwa wanakiuka  utaratibu  wa halmashauri  wa kubeba  abiria  nje  ya kituo kipya.

Kutokana na kukamatwa na kutozwa faini madereva hao wameiomba Serikali wilayani humo kuwatazama kwa jicho la tatu kwa kuwaruhusu kutumia stendi ya zamani kupakia na kushusha abiria kwa kuwa katika stendi mpya hawapati wateja wengi.

Dereva Hassan Amiri na Fredrick Ruangisa  wamesema endapo gari la dereva litabainika kuwa na makosa ni vyema watendaji wa halmashauri ya mji wa Nzega wakatoa taarifa kituo cha Polisi kwa kuwa askari ndio wenye mamlaka ya kukamata magari na si vinginevyo.

"Tunaomba kwa yeyote mwenye dhamana watusaidie turudishwe stendi ya zamani huko ndio rafiki kwetu tunapata wateja wengi," amesema Hassan

Kwa upande wake Zungu Joseph na Lucas Lusumo ambao ni wamiliki wa magari madogo wameisisitiza Serikali kuwatazama kwa jicho la huruma ili warudishwe stendi ya zamani kupakia na kushusha abiria.

Kutokana na malalamiko hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magesa amesema msimamo  wa halmashauri hiyo ni kusimamia  kanuni  na taratibu  iliyojiwekea.

Amefafanua kuwa kwa sasa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) Mkoa wa Tabora wapo wilayani humo kwa ajili ya kuzipaka rangi gari ndogo zinazofanya safari za mizunguko ya ndani.

Aidha imeelezwa kuwa Halmashauri  ya  mji  wa  Nzega  ilifanya  uamuzi  wa  kujenga  stend mpya  ya  mabasi  ili  kupanua  wigo  wa  ukusanyaji mapato  ya  Serikali  kwa mwezi na ikajiwekea  utaratibu  kwa  magari  yote  yanayobeba  abiria  kuhamishiwa  katika  stend  hiyo  mpya  ya mabasi  hatua  ambayo  imekuja  kusababisha  mzozo  baina  yake  na madereva  wa magari madogo,  wakidai  kuwa  stend  hiyo  mpya  wanakosa  abiria  wa  kutosha  kama ilivyo  kwa  stend  ya  zamani  waliyoizoea  ambayo  ipo  mjini.i.
Magari  madogo ya abiria ya Noah na Hiace
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega,Philemon Magesa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...