Picha za michoro ya nyumba ya Makamu wa Pili wa Rais ambayo inajengwa Pagali Shehia ya Mkoroshini, Chake Chake Pemba ambapo jiwe la msingi wa ujenzi wa makazi hayo limewekwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Tukufu Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi kuashiria zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar limekamilika, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud, makazi hayo yanajengwa katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msanifu wa Majengo kutoka Ofisi ya Wakala wa Majengo Bi. Hawa Natepe mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.
Wachezaji ngoma za asili wakionyesha umaridadi kwa kucheza ngoma ya Kilumbizi yenye asili ya Pujini wilaya ya Chake Chake Pemba wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais katika eneo la Pagali, Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutumia Vikosi vyake katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Makamu wa Rais ametoa pongezi zake leo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mkoroshoni Chake Chake Pemba.

Hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ni sehemu ya shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ambayo kilele chake itakuwa Jumamosi tarehe 12 Januari, 2019.

“Sote tutakumbuka kuwa wakati wa kupigania uhuru wetu Chama cha Afro Shirazi Party (ASP) kiliwaahidi wananchi wake kuwajengea makaazi bora yenye heshima ya utu. Ahadi za ASP zimerithiwa na Chama cha Mapinduzi na ndio maana leo hii tupo hapa kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la makazi bora ya mwananchi mwenzenu, kiongozi wetu, Makamu wa Pili wa Rais”. Alisema Makamu wa Rais.

Ujenzi huo wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.6 za kitanzania.
Kwa Upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali imeweka umuhimu katika kujenga makazi ya watumishi wake pamoja na Ofisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...