Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumchukua aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa ili kwenda kuwahoji.

Maombi hayo, yamewasilishwa mahakamani hapo leo Januari 16, 2019  na Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka lakini wakili Swai ameieleza mahakama kuwa mashahidi waliotarajiwa kufika leo wamepata udhuru, ambapo mmoja anaumwa na mwingine amepangiwa kazi Utumishi.

Aidha Swai ameiomba mahakama hiyo amchukue Malinzi na Mwesigwa kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano Takukuru kwa sababu kuna vitu wanataka kuviongezea. Kufuatia hayo, upande wa utetezi wameiomba mahakama ichukulie suala hilo kwa uzito kwa sababu washtakiwa wapo ndani wanateseka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi. Mbali ya Malinzi na Mwesigwa, washtakiwa wengine ni Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga, Meneja wa ofisi ya TFF, Miriam Zayumba na Karani Frola Rauya.

 Katika  kesi hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 katika kesi hiyo washtakiwa wote kwa pamoja pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30
yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...