Khadija Khamis – Maelezo  Zanzibar
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Ibrahim Raza amesema ushirikiano wa wananchi na viongozi wa jimbo ndio hatua bora inayoleta ufanisi wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinatekelezwa kwa vitendo. Aliyasema hayo huko katika kiwanja cha mpira cha Kwala, Mombasa, wakati akizungumaza na waandishi wa habari walipofika kuangalia Taa zilizowekwa katika kiwanja hicho na kukiwezesha kutumika wakati wa usiku

Taa hizo zimewekwa kwa ajili ya kuwapa fursa vijana kucheza wakati wote na kukuza vipaji walivyanavyo na hatimae kupata nafasi ya usajili kwa vilabu vikubwa.  Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mahamoud Thabit Kombo alisema baada ya kiwanja hicho kuwekwa taa, wanampango wa kukiimarisha zaidi kwa kukiweka nyasi badia.

Alisema lengo ni kuimarisha michezo katika jimbo la Kiembesamaki ikiwa ni moja ya njia ya kutengeneza ajira kwa vijana na kuwaepusha na vitendo viovu. Aliwataka vijana wanaoishi karibu na kiwanja hicho kuwa walinzi wa raslimali iliyowekwa ili kidumu kwa muda mrefu na kiweza kutumiwa na vizazi vya sasa na vinavyokuja

Mwenyekiti wa C.C.M Jimbo la Kiembe Samaki Ramadhani Mrisho Rupia alisema kuimarisha michezo ni moja ya ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuwasaidia vijana kujiajiri kutokana na vipaji walivyonavyo. Taa za kiwanja cha mpira cha Kwala zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 22, mwaka huu kwa mechi maalum itakayofanyika wakati wa usiku.

Nae kijana Nasir Ali Hemed  Mkaazi wa kwa Mchina ambae ni mmoja ya vijana wanaotumia kiwanja cha Kwala , alisema amepata faraja  kuona viongozi wao wametekeleza ahadi zao kwa vitendo. Aliwaomba viongozi wa Jimbo hilo kuwapatia mashine ya kukoshea gari (Presha Pampu) ili vijana waweze kujiajiri wenyewe. Jumla ya shiling milion 20 zimetumika kwa ajili ya kuweka miundombinu ya umeme katika kiwanja hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki ambae pia ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo na Mbunge wa Jimbo hilo Ibrahim Raza pamoja na Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Ramadhan Mrisho Rupia wakizungumza na wandishi wa habari walipokua wakikagua kiwanja cha Mpira cha Kwala Mombasa Kwamchina kilichowekwa Taa. Picha na Makame Mshenga.
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza akizungumza na vijana wa Jimbo hilo alipofika kukagua Taa zilizowekwe kwenye uwanja wa Mpira wa Kwala Mombasa kwa Mchina Mjini Unguja. 
 Kijana Nasir Ali Hemed akiwashukuru Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki kwa kutekeleza ahadi zao walizoweka wakati wa kampeni. 
  Muonekano wa kiwanja cha mpira cha Kwala na moja ya Taa zilizowekwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki ikiwa ni miongoni mwa ahadi walizozitoa wakati wa Kampeni. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...