Na Ripota Wetu,Tunduru

MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amepokea ng'ombe zaidi ya 200 kutoka kwa wafadhili na kuzigawa katika kaya za wilaya hiyo katika kata 16 na vijiji 64 vinavyotekelezewa mradi wa Boresha afya ya mama na mtoto (AMCC) maarufu CHIP chini ya ufadhili wa Kanisa Anglican dayosisi ya Masasi.

Homera amekabidhi ng'ombe hizo jana ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua ni vema wananchi wakatunza mifugo hiyo ili kupata tija katika kuinua maisha yao.

Amefafanua hadi sasa zaidi ya Sh. million 405 zimetumika katika programu ya kopa ng'ombe lipa ng'ombe na kaya nyingi zimenufaika na mpango huo huku akisisitiza kwa kuwaeleza wananchi wahakikishe ng'ombe hizo zinatunzwa kama ambavyo inafanyika kwa wananchi ambao tayari walishapatiwa ng'ombe hao ambao wanatolewa bila gharama yoyote zaidi ya mhusika kutengeneza banda la kufugia tu.

Aidha Mkuu wa Wilaya Homera alieleza pia huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 ibara ya 25 kifungu (f). Pia pamoja na mifugo hiyo pia kupitia mpango huo wananchi wamenufaika na mbuzi wa Maziwa,Kuku,Bata,Kondoo,Kanga,na Sungura .

Hivyo amesema wananchi wanaimarisha afya zao kutokana na kupata kitoweo na maziwa na kuendelea kupunguza wimbi la changamoto ya utapiamlo na udumavu kwa kuzingatia kanuni za lishe bora.

Ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi wote wa Wilaya ya Tunduru kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo huku akitoa shukrani zake kwa Kanisa hilo ambalo limeamua kujikita katika kuona jamii inanufaika na uwepo wao kupitia mradi huo.

Ameongeza kuwa Kanisa hilo mbali ya kutoa mifugo kwa wananchi pia limesaidia jamii ya Wana Tunduru kwa kuchimba visima vya maji 25 ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanashiriki kufanikisha maji yanapatikana.

"Niwapongeze zana meneja wa mradi huo pamoja na timu yako yote kwa uamuzi wenu wa kushirikiana nasi wananchi wa Tunduru katika kuleta maendeleo," amesema Homera.
MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amepokea ng'ombe zaidi ya 200 kutoka kwa wafadhili na kuzigawa katika kaya za wilaya hiyo  katika kata 16 na vijiji 64 vinavyotekelezewa mradi wa Boresha afya ya mama na mtoto (AMCC) maarufu CHIP chini ya ufadhili wa Kanisa Anglican dayosisi ya Masasi.

Mh Homera amesema mpaka sasa zaidi ya Sh. million 405 zimetumika katika programu ya kopa ng'ombe lipa ng'ombe na kaya nyingi zimenufaika na mpango huo, huku akisisitiza kwa kuwaeleza wananchi wahakikishe ng'ombe hizo zinatunzwa kama ambavyo inafanyika kwa wananchi ambao tayari walishapatiwa ng'ombe hao ambao wanatolewa bila gharama yoyote zaidi ya mhusika kutengeneza banda la kufugia tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naomba kusaidia tu kunyoosha kiswahili. Tuseme ng'ombe hao, siyo ng'ombe hizo! Vilevile wale viongozi kule Dallas wamejiuzulu, siyo kujiudhuru!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...