Na Shani Amanzi, Chemba.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga amachukizwa na Wananchi na Wafanyakazi wa Serikali wasiokuwa wawijibikaji hasa pale wanapopewa majukumu na Serikali ikiwemo kuwekwa kwenye Kamati za shughuli za kimaendeleo katika jamii.

Mhe. Odunga aliyazungumza hayo alipotembelea kata ya Mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo. 

 “Nampongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuweka kipaumbele katika Afya na kutaka kila kata kuwe na Kituo cha Afya na sitakubali mwananchi au mtaalam yoyote akwamishe malengo hayo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa”, alisema.

Aidha Mhe.Odunga aliongeza kwa kusema mkumbuke wapo Wananchi ambao baadhi yao wapo macho na wanataka kushirikishwa katika kila jambo na inasikitisha sana Kamati hii ya Ujenzi inafanya mambo bila kuwashirikisha Wananchi na ninaamuru Kamati hii ivunjwe na kutaka Mkurugenzi ahakikishe anaunda nyingine mara moja kuanzia leo kwani wengi wao wananchi hawaiamini Kamati hii ikiwemo na upande wa manunuzi. 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus.H.Mashimba ameomba ushirikiano kwa Wananchi katika kuhakikisha Ujenzi wa Kituo cha Afya- Mrijo kinakamilika na kuipongeza Serikali katika kuweka kipaumbele Chemba katika Ujenzi wa Vituo vya Afya. 
 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga wa pilia kushoto akizungumza na wananchi (hawapo pichani)  baada ya kuitembelea kata ya Mrijo akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri (wa pili kulia) Mh.Dkt.Semistatus Mashimba  pamoja na Katibu Tawala Zahara Muhidin Michuzi (mwisho kushoto) sambamba na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019. 
 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza na baadhi ya Wananchi  alipotembelea kata ya mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019. 
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mrijo wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nano baada ya kuitembelea kata ya mrijo akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri, Mh.Dkt.Semistatus Mashimba  pamoja na Katibu Tawala Zahara Muhidin Michuzi sambamba na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...