Mtanzania, Mohamed Mansour Nassor anaetokea Zanzibar ambae anafanya masomo kiwango cha juu ya PhD katika fani ya Uchumi ambae pia ndio Raisi wa Umoja wa Vijana na Wanafunzi wa Nchi zote za Afrika(ASSAFSTU) katika Chuo Kikuu kwa Jina maarufu la Patrice Lumumba(RUDN University) ametunukiwa tunzo kubwa ya Kimataifa kwa Kuhamasisha vijana wa nchi za Afrika nchini Urusi.


Na ujumbe wake ulisema kama ifuatavyo:



Leo tarehe 12/01/2019 kwa uwezo wa Mungu nimefikia tena kutambuliwa Kimataifa na najivuna tumeendelea tena kulitangaza vyema Taifa letu la Tanzania katika anga za Kimataifa. 

Kwa heshima kubwa kwangu na kwa nchi yetu, nimetunukiwa Tunzo ya kufanya vyema sana katika kuhamasisha vijana wa Afrika nchini Urusi katika masuala ya Taaluma(Elimu) na Maendeleo ya Jamii(Community Development) kupitia Shirika la vijana wa Kiafrika lisilo la Kiserikali(NGO) la Youth of Large Exploit(YOLE) katika hafla yao iliofanyika mjini Moscow.
Kwa uwezo wa Mungu, pamoja na tunzo huu ya leo tayari inakua ni kwa mara pili kutambuliwa Kimataifa kwa mwaka huu wa 2019 tangu uanze ambapo pia mwezi huu wa Januari nilichapishwa na kutambuliwa Kimataifa kama Mtanzania maarufu zaidi katika Watanzania waliowahi kusoma vyuo vya Sovieti ya Urusi na Urusi katika jarida la Kimataifa(Encyclopedia) la Wahitimu wote wa kigeni waliosoma nchini Urusi yani SOYUZ Alumni. 

Lakini si hivyo tu Tarehe 11 Mwezi Novemba 2018 nilifikia hatua kubwa katika masuala ya uongozi Kimataifa ambapo nilichaguliwa kuwa Raisi wa Vijana wote wa Nchi za Afrika katika Chuo Kikuu Cha Urafiki Cha Watu Wa Urusi au maarufu kama Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba ambapo nafasi hii ndio kwa mara ya Kwanza inshikwa na Mtanzania tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki miaka ya 1960. 
Aidha licha ya hivyo bado, nimekua nikifanya kazi za uongozi kama Makamu Mwenyekiti wa Diaspora ya Watanzania nchini Urusi na nchi za CIS yani TADIRU na kama Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kiswahili Cha Moscow(CHAKIMO) chini ya Ulezi wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Urusi,Mheshmiwa Simon Marco Mumwi. Namshukuru sana mheshimiwa Balozi wetu na Ubalozi kwa ujumla kwa mwongozo, nasaha, usahuri na kunipa dira na kunipa msaada mkubwa katika majukumu yangu na harakati zangu.
Nawashukuru sana viongozi wa shirika la YOLE na pia Chama chetu Cha SOYUZ Alumni Association of Tanzania walioniamini ili kuwawakilisha Kimataifa kama Balozi wao. 

Napenda pia kuwashukuru Watanzania wote wanaounga mkono juhudi zangu na harakati zangu na kwa dua zao njema kwangu hasa kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania linaloongozwa na Raisi Makini kabisa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
Ahsante sana!  





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...