NA ALFRED MGWENO TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amefanya ziara katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kuwataka wafanyakazi wa Wakala huo katika mikoa hiyo kuongeza juhudi katika kazi ili kuhakikisha wanazalisha kipato cha kutosha kuweza kufikia malengo au hata kuzidi mapato waliyojiwekea kwa mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.

Akizungumza na wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti, Mhandisi Maselle alisema anatambua kwamba TEMESA inakumbwa na changamoto nyingi za kiutendaji ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi hasa vya karakana pamoja na upungufu wa wafanyakazi lakini aliwataka mameneja wa mikoa hiyo pamoja na watumishi wake kujitahidi kufanya kazi zao kwa ufansi na kwa ushirikiano huku akiangalia namna ya kuwaongezea vitendea kazi na kujaza nafasi za watumishi zilizoachwa wazi baada ya kustaafu.


Katika mazungumzo yake Mhandisi Maselle alisisitiza kwamba, Kiongozi mzuri ni yule ambaye anafanya kazi bega kwa bega na wafanyakazi wenzake pale anapoona mapungufu na kuwatia moyo hivyo meneja ajitahidi kuwa karibu na watumishi wake.

Awali, Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo, alimpitisha Mtendaji Mkuu katika karakana ya mkoa ambapo alipata nafasi ya kukagua mashine na mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana hiyo na baadae alimkaribisha katika kikao na watumishi na kumkumbushia kuhusu changamoto zinazoukumba wakala kubwa likiwa ni upungufu wa wafanyakazi ambapo karibu kila kitengo kina mtumishi mmoja mmoja ikiwemo kitengo cha uhasibu na kitengo cha manunuzi na kumuomba kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha watendaji wa mkoa huo wanapata wasaidizi ili waweze kutenda kazi zao kwa ufanisi.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya kuchongea vipuri vya injini za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akielezea jinsi mashine ya kubadilishia tairi za magari inavyofanya kazi wakati akikagua mashine mbalimbali zilizopo katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akitoa maelekezo kwa mafundi na wafanyakazi wa karakana ya mkoa wa Arusha mara baada ya kukagua mtambo wa kuchenjua na kuchakata kokoto (Crusher) unaoonekana pichani.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati (aliyevaa koti) akikagua mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana ya wakala huo mkoani Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...