Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema Spika wa Bunge akimuita mtu lazima aende.
Ametoa
kauli hiyo leo Januari 18,2019 mbele ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa
hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kuratibu na kudhibiti
Mawasiliano(TTMS) yaliyofanyika Mamlaka yaMamlaka ya Mawasiliano
Tanzania(TCRA).
Sheikh
Alhad wakati anaomba dua kwa ajili ya viongozi wa ngazi mbalimbali
nchini alianza kwa kumuombea Rais Magufuli, Makamu wa Rais Samoa Suluhu
Hassan ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge.
"Mwenyezi
Mungu tunakuomba uumpe afya njema Spika wetu wa Bunge mzee Ndugai.Huyu
Spika akimuita mtu lazima aende," amesema Sheikh Alhad huku baadhi ya
watu waliokuwa wanasikiliza dua yake kuanza kucheka.
Haikufahamika
mara moja walikuwa wanacheka nini lakini ukweli kauli ya Sheikh Alhad
inakuja kipindi ambacho kunamjadala baada Spika Ndugai kumuita Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)Profess Mussa Assad katika Kamati ya
Bunge ya Kinga,Haki na Maadili ili ahojiwe baada ya kuelezea Bunge ni
dhaifu.
Hata hivyo wakati
Sheikh Alhad akisema kwamba mtu akiitwa na Spika Ndugai lazima aende
inakuja kipindi ambavyo tayari CAG Profesa Assad amethibitisha ataitikia
mwito wa Spika Januari 21 mwaka huu.
Kwa
upande wa Spika jana wakati anazungumza na waandishi wa habari amesema
ana uhakika Profesa Assad atakwenda kwenye kamati kuhojiwa ili apate
fursa ya kuwasilisha utetezi wake na kwamba iwapo hatafika atajua nani
muajiri wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...