Watu watatu wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe, wakishtakiwa kuiba mkoba uliokuwa na $150,000 (£117,600) pesa taslimu mali ya rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe.

Washukiwa hao wa wizi wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo.

Jamaa wa rais huyo wa zamani, Constantia Mugabe, ni miongoni mwa walioshtakiwa, kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya serikali.

Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na funguo za nyumba ya kijijini ya Bw Mugabe iliyo eneo la Zvimba karibu na mji mkuu wa Harare, na ndiye aliyewasaidia hao wengine kuingia humo na kufika ulikokuwa mkoba huo.

Washukiwa hao wengine walikuwa wameajiriwa kama wafanyakazi wa kufagia na kusafisha nyumbani humo wakati wa kutekelezwa kwa wizi huo siku moja kati ya tarehe 1 Desemba na mapema Januari.

"Johanne Mapurisa alinunua gari aina ya Toyota Camry... na nyumba ya $20,000 baada ya kisa hicho," mwendesha mashtaka wa serikali Teveraishe Zinyemba aliambia mahakama ya hakimu eneo la Chinhoyi."Saymore Nhetekwa alinunua gari aina ya Honda... na mifugo wengine wakiwemo nguruwe na ng'ombe wa thamani ambayo haijulikani."

Bw Mugabe, ambaye kwa sasa ana amiaka 94, aliondolewa madarakani na jeshi la Zimbabwe kwama 2017.Kufikia wakati wa kufurushwa madarakani, alikuwa amekaa madarakani kwa miaka 37, mwanzoni kama waziri mkuu na baadaye kama rais wa taifa hilo.

Wakati mmoja anakumbukwa kwa kusema kwamba taifa lolote lile haliwezi kufilisika.

CHANZO BBC Swahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...