Daktari Bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akimweleza  Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera maendeleo ya afya ya mtoto aliyefanyiwa  upasuaji wa bila kufungua kifua na kuzibwa matundu ya moyo katika kambi   maalum ya matibabu inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo kwa watoto wa  JKCI, Israel na Ujerumani.
 Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini,  Jörg Herrera akiangalia uzibuaji wa mishipa ya moyo iliyoziba jinsi unavyofayika  katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuuguzi  Robert Mallya akimweleza Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera kuhusu mendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel Simon Fisher na kulia ni Afisa Mipango wa JKCI Vida Mushi.
 Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na wafanyakazi wa JKCI , Israel na Ujerumani mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua.
Balozi  Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua katika kambi hiyo ya siku tano.Picha na JKCI.


========  ==========  ============ ========

Ubalozi wa Ujerumani kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.


Ubalozi wa Ujerumani nchini umeahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuleta wataalamu wa magonjwa ya moyo ikiwa ni njia moja wapo ya kubadilishana uzoefu na ujuzi katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa watoto wenye matatizo ya moyo.

Ahadi hiyo imetolewa leo na Kaimu Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Jörg Herrera alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani.

Mhe. Balozi Herrera alisema madaktari kutoka nchini Ujerumani wanauzoefu wa kutosha wa kufanya upasuaji kwa watoto wenye umri mdogo kuanzia siku moja, hivyo ujio wao utakuwa na manufaa kwa madaktari wa JKCI kwa kuweza kubadilishana ujuzi wa kazi wa kutoa matibabu ya kibingwa kwa watoto.

“Katika kambi hii kuna daktari kutoka Ujerumani mwenye uwezo wa kumfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua mtoto mwenye umri wa siku moja, ujuzi huu ukisambazwa kwa madaktari wengi utasaidia kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo wanaopoteza maisha katika umri mdogo,” alisema Mhe. Herrera.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kambi ya madaktari kutoka nchini Israel na Ujerumani imeweza kuokoa maisha kwa watoto ambao wamefanyiwa upasuaji na kuongeza ufanisi kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo.

Aidha Prof. Janabi aliushukuru ubalozi wa Ujerumani kwa kuendelea kushirikiana na JKCI na kutuma wataalamu wake ambao wamekuja hapa nchini kutoa huduma ya matibabu kwa watoto.

“Ujuzi tunaoendelea kuupata kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa magonjwa ya moyo kupitia kambi maalum za matibabu ikiwemo madaktari kutoka nchini Ujerumani zinatusaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya moyo,” alisema Prof. Janabi.

Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo kuziba na kutopitisha damu vizuri wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua katika kambi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri huku wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...