Na Munir Shemweta, Dodoma
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula ameridhishwa na maendeleo ya
ujenzi wa ofisi za wizara katika mji wa serikali ya Mtumba mkoani Dodoma
unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Dk Mabula alitoa kauli
hiyo leo tarehe 22 Januari 2019 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi
za Serikali katika mji wa Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) ambalo liko chini ya Wizara yake.
Alisema kazi
inayofanywa na shirika la Nyumba la Taifa kujenga ofisi za Serikali katika mji
huo kwa sasa unaenda kwa kasi na unatia moyo jambo linalooonesha kuwa mradi wa
ujenzi wa ofisi hizo utakamilika katika muda uliopangwa.
Katika mradi huo Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi inajenga ofisi za
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Uchumi,
Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Dk Mabula
amefurahishwa na ufuatialiaji wa ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Wizara ya
Fedha pamoja na Viwanda na Biashara na kueleza kuwa hatua hiyo inalifanya
Shirika hilo kufanya kazi kulingana na mahitaji ya wateja wake.
Alibainisha kuwa,
pamoja na changamoto ya kukatika umeme lakini NHC imejitahidi na
kilichomfurahisha ni kuwepo vifaa vyote vya ujenzi kwenye eneo la ujenzi jambo
linalompa faraja kuwa hakuna kitakachokwamisha ujenzi kukamilika kwa wakati
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi amepongeza jitihada znazofanywa na Rais John
Pombe Magufuli za kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma na kubainisha kuwa
hatua hiyo inatimiza ndoto ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Naye Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Emma Lyimo alilisifu
Shirika la Nyumba la Taifa kwa kasi kubwa wanayoendelea nayo kwenye ujenzi wa
ofisi ya Wizara yake na kubainisha kuwa pamoja na kuchelewa kuanza ujenzi
lakini kasi wanayoenda nayo ana imani ujenzi utakamilika kwa wakati.
Naye Msimamizi wa
ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo la Makazi Mhandisi Grace
Musita alisema, ujenzi wa ofisi umefikia asilimia sabini na tano na anatarajia
utakamilika katika tarehe iliyopangwa kwa kuwa wamefikia
hatua nzuri ya kukamika.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula
akiangalia maendeleo ya Ujenzi ya Ofisi ya Wizara ya Nishati katika mji wa
Serikali wa Mtumba, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la
Taifa Elisante Ulomi na katikati ni meneja mradi Haikameni Mlekio.
Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akioneshwa moja ya
kifaa kitakachotumika katika Ujenzi ya Ofisi ya Wizara ya Nishati katika mji wa
Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma, kulia ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la
Nyumba la Taifa Elisante Ulomi na kushoto ni meneja mradi Haikameni Mlekio.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akimsikiliza
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Bisahara Emma
Lyimo (Kulia) wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Viwanda
na Biashara katika mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma, kushoto ni Mhandisi
wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Hassan Mohamed.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dk Angelina Mabula akiongozwa na Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la
Nyumba la Taifa Grace Musita kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali eneo la Mtumba Dodoma .
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula katikati
akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali wa Mtumba kutoka kwa meneja mradi wa
Shirika la Nyumba Haikameni Mlekio wakati alipofanya ziara, kushoto ni Mhandisi
wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akipata
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi katika mji wa Serikali wa Mtumba kutoka kwa meneja mradi wa Shirika
la Nyumba Haikameni Mlekio (kulia) wakati alipofanya ziara, kushoto ni Mhandisi
wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...