Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) Mhe. Anthony Mavunde ameutaka uongozi wa Kazi SACCOS kubuni miradi yenye tija ili kuboresha mfuko wao na kuleta manufaa kwa wanachama wake. Ametoa rai hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanachama wa SACCOS hiyo uliofanyika Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.

Ameutaka uongozi wa chama hicho kubuni miradi ya kimkakati inayotekelezeka na kuendana na mazingira, na hali ya kiuchumi ya eneo husika. “Ni vyema uongozi kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo Dodoma ili kuanzisha miradi itakayoendana na hali halisi ya kiuchumi pamoja na kukikwamua chama chenu kuendelea kuwa na tija,” alisisitiza Mavunde.

Lengo la mkutano hilo lilikuwa ni kupeana taarifa za uendeshaji wa chama, kufanya uchaguzi wa viongozi wapya katika bodi ya uongozi na kamati ya usimamizi pamoja na kujadili namna bora ya kuendelea kuboresha Chama hicho ili kuendelea kuwa na tija kwa wanachama wake.

Aidha aliwatoa hofu wanachama kwa kueleza kuwa, uwepo wa vyama hivi ni kisheria na kikanuni za utumishi wa umma na kuwataka kuviheshimu ili kuendelea kuwa wanachama hai. “Ieleweke kuwa ukiwa katika chama hiki, bado upo katika utaratibu na kanuni za utumishi wako hivyo muendelee kufanya vyema katika chama ili kujipatia heshima ndani na nje ya ofisi yako,” alisema Mavunde.

Aliwapongeza viongozi pamoja na wanachama wote kwa mchango wanaoutoa kwa ofisi yake kuzingatia mchango wa Chama kwa watumishi wote. “Ninashawishika na kuona mchango wenu kwetu kama ofisi, kwani mmechangia kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wetu, ambao vinginevyo wangeshindwa kutoa huduma bora yenye tija kwa wadau wetu kutokana na changamoto za kifedha huwenda ingechangia kuwaingiza katika matendo ya utovu wa nidhamu kama vile rushwa”,alisisitiza Mavunde.

Pia aliwataka viongozi wa Ofisi yake kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ambazo chama kimezionesha hususani uanzishwaji wa miradi ikiwemo ikiwemo kuwekeza katika viwanda. Naye Omari Sama mwenyekiti wa chama hicho aliunga mkono maagizo hayo kwa kuanzisha miradi endelevu itakayoleta maendeleo ya kiuchumi kwenye chama, kuongeza wanachama na kukifanya chama hiko kitambulike zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Peter Kalonga aliuasa uongozi mpya kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwa wanachama ili kuweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Kazi SACCOS Ltd walipokutana Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.
 Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Dorothy Uwiso akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Kazi SACCOS Ltd walipokutana Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Kazi SACCOS Ltd wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akifuatilia Taarifa ya Utekelezaji ya Bodi ya Uongozi wa Kazi SACCOS LTD wakati wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Kazi SACCOS Omari Sama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Bodi ya Uongozi wa Kazi SACCOS LTD wakati wa Mkutano Mkuu wa SACCOSS hiyo Januari 19, 2019 Ukumbi wa TAKWIMU Dodoma.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Peter Kalonga akiwasilisha salamu za Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ambaye ndio Mlezi wa Chama wakati wa mkutano huo.
 Baaadhi ya wanachama wa Kazi SACCOS wakifuatili uwasilishwaji wa mada kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Kazi SACCOS Omari Sama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
 Afisa Kazi Wilaya ya kinondoni  Yusuf Nzugile akichangia mada wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu Wanachama wa Kazi SACCOS Januari 19, 2019.Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...