NA.LUSUNGU HELELA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

Ameyabainisha hayo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo. “Kazi hii inafanywa kwa uhodari mkubwa, nawapongeza kwa maendeleo yaliyofikiwa na ninaamini kwamba Jengo hili litakamilika ndani ya muda uliopangwa’’

Aidha, Mhe. Kanyasu wakati alipotembelea eneo hilo ameweza kukutana na timu ya Wakadiliaji Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao kwa pamoja na Fundi Sanifu Ujenzi, Agastoni Kayugwa ambaye ni Muwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja wameeleza kuwa wanaridhishwa na spidi inayoendelea katika ujenzi wa jengo hilo.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa SUMA JKT, Luteni Mturi amemueleza Naibu waziri huyo kuwa wanatarajia kumaliza ndani ya muda uliopangwa kwa vile kwa sasa kuna upatikanaji wa uhakika wa vifaa vya ujenzi ikiwematofali ya kutosha na yenye ubora wa hali ya juu pamoja na wafanyakazi wa kutosha

‘’Kesho tunategemea kuanza kumwaga zege katika kipande cha kwanza ambapo hadi kesho kutwa tutamalizia kipande cha pili’ ameeleza Mturi. Hata hivyo, Mkandarasi huyo ameeleza changamoto ya utayari wa wafanyakazi kufanya kazi usiku kuwa wengi wao wamekuwa hawapo tayari kufanya kazi muda huo licha ya kuwa awali SUMA JKT ilipanga kujenga jengo hilo mchana na usiku.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiangalia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo hilo katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akizungumza na Mkandarasi wa Suma JKT, Luteni Mturi wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma., kushoto ni Fundi Sanifu Ujenzi, Agastoni Kayugwa ambaye ni Muwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja wameeleza kuwa wanaridhishwa na spidi inayoendelea katika ujenzi wa jengo hilo. 
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya jengo jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...