Na Chalila Kibuda, Moshi

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetajwa kuwa nguzo muhimu katika uimarishaji wa huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali nchini.

Akizungumza na Maofisa Uhusiano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda KCMC, Gileard Masenga alisema kuwa mchango wa NHIF umekuwa ni mkubwa katika upande wa mapato pamoja na uimarishaji wa miundombinu na vifaa tiba.

"Kwa kweli niseme ukweli kabisa NHIF kwetu ni uti wa mgongo katika uendeshaji wa shughuli zetu na ndio maana kila siku nikikutana na Mkurugenzi Mkuu Konga huwa namwambia watulindie sana huu Mfuko maana umekuwa mkombozi mkubwa sana katika sekta ya afya," alisema Dkt. Masenga.

Alieleza kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa katika eneo la wagonjwa wa dharula hospitalini hapo yanatokana na NHIF. " Kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika eneo zuri na lenye nafasi ikilinganishwa na awali," alisema.

Kwa upande wa Meneja wa wa NHIF Mkoa wa Arusha, Isaya Shekifu amesema kuwa Mfuko umekuwa na mpango wa uimarishaji wa miundombinu na upatikanaji wa vifaa tiba kupitia fursa ya mkopo nafuu kwa lengo la kuboresha huduma za matibabu.Shekifu amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Awamu ya Tano, NHIF imekuwa na Mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma kwa wanachama wake ikiwemo kuwafikia wananchi katika maeneo yao.

Alisema kuwa usogezaji wa huduma kwa kuwa na ofisi kila Mkoa umesaidia kutoa huduma bora kwa wananchi na kupanua wigo wa wanachama lengo likiwa ni kuwafikia asilimia 50 ya wananchi ifikapo mwaka 2020."Tumejipanga vizuri kutokana na serikali awamu ya tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwekeza kwa nguvu katika sekta ya afya hatutarudi nyuma na kumwachia Rais Mwenyewe...lazima tuwafikie wananchi ili waweze kupata huduma kirahisi kupitia NHIF," amesema Shekifu.

Naye Afisa Uhusiano wa NHIF, Grace Michael alitoa wito kwa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote."Mfuko umejipanga vizuri kuhakikisha unafika kijiji kwa kijiji ili kila Mtanzania apate elimu ya Bima ya Afya na hatimaye ajiunge na kwa kufanya hivyo atakuwa na uhakika wa kupata matibabu na uhakika wa kutunza Afya yake," alisema Grace.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NHIF akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea ofisi ya Kanda mkoani Arusha.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Grace Michael akizungumza katika ofisi ya Kanda ya NHIF mkoani Arusha wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea ofisi hiyo ikiwa ni Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya inayofanywa Maafisa hao.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Isaya Shekifu akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati walipotembelea Ofisi ya Kanda hiyo mkoani Arusha ikiwa ni kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa ni Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya ya Maafisa hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...