Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

RAIA wa Pakistani, Muhammad Hasnaih Hyderi leo Januari 17,2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutaka kumpa rushwa Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Imedaiwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru), Pascal Magabe akisaidiana na wakili, Leornad Swai kuwa, Januari 15, 2019 huko katika Mgahawa wa Best Bite uliopo ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa alitoa rushwa ya Sh. milioni mbili kwa Talib Kombo ambaye ni Ofisa wa TRA)  ili kumsaidia asilipe kodi kubwa.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande Kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kuwa na wadhamini wawili kutoka ofisi yoyote inayotambulika na Serikali watakaosaini bondi ya Sh.milioni tano kila mmoja.

Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria na haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es  Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.Kwa mujibu upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umeisha kamilika na kesi hiyo itatajwa Januari 31 mwaka huu
MtuhumiwaRAIA wa Pakistani, Muhammad Hasnaih Hyderi leo Januari 17.2019 akifikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutaka kumpa rushwa afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...