Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

VIONGOZI wa dini mbalimbali nchini wamesema wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli kwa kudhihirisha namna ambavyo inatambua na kuthamini uwepo wa viongozi wa dini na kuwapa nafasi.

Wakizungumza leo Januari 18,2019 wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano TTMS yaliyofanyika eneo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ambapo mgeni rasmi ni Rais Dk.John Magufuli.

Viongozi hao wamemwambia Rais Dk.Magufuli kuwa tangu ameingia madarakani viongozi wa dini wamekuwa wakipewa nafasi kubwa na ya kuheshimiwa na hivyo wanamshukuru kwa namna ambavyo amewapa nafasi hiyo.Wamesema kwa nyakati tofauti viongozi wa dini wamekuwa wakijadiliana namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano ambavyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na viongozi hao wa dini.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhad Mussa Salum amesema Rais Magufuli amewapa nafasi kubwa viongozi wa dini kuliko kipindi chochote kile."Hakika viongozi wa dini tunayo sababu ya kukiri utawala huu wa Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa karibu nasi,tunashirikishwa kwenye mambo mbalimbali.

"Hivyo wamekubaliana kutambua kuwa Serikali ya inayoongozwa na Rais Magufuli imeamua kuwaweka karibu viongozi wa dini," amesema Sheikh Alhad na kuongeza viongozi wa dini wataendelea kumuombea yeye na viongozi wengine wa Serikali na wananchi wote kwa ujumla.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Full Gospell Bible Zacharia Kakobe amesema anaungana na Sheikh Alhad kwa kuelezea kuhusu namna ambavyo viongozi wa dini wanapewa kipaumbele kwenye Serikali.Amefafanua Rais Magufuli ameonesha unyenyekevu mbele ya viongozi wa dini na kwake madhehebu yote ya dini kwake yako sawa,hakuna dhehebu kubwa wala dogo.

"Rais kabla kuja hapa mbele wakati tumekaa pale tulikuwa tunajadiliana namna ambavyo umetoa kipaumbele kwa viongozi wa dini.Tunakushukuru kwa uamuzi wako wa kuwa karibu na viongozi wa dini," amesema Askofu Kakobe.

Kila viongozi wa dini ambaye alipata nafasi ya kukaribishwa kuomba dua alitumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Rais Magufuli amekuwa na hofu ya Mungu na amekuwa akimtanguliza Mungu kwa kila jambo na ndio maana amekuwa akifanikiwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zacharia Kakobe  katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...