Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe wakipewa maelezo na  Rubani Patrick kuhusu ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 walipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakiwa na viongozi wengine mbalimbali wakishuka kutoka katika ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 ilipowasili na kupokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.
 Maafisa waliokwenda Canada kuipokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 wakilakiwa kwa shangwe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
Picha na IKULU
 Ndege mpya ya kisasa aina ya Airbus 220-300 iliyopewa jina la moja ya hifadhi ya  mbuga za wanyama  (Ngorongoro), ikikaribishwa kwa water salute mara baada ya kutua leo 11 Januari 2019 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere  ikitokea Canada ilikotengenezwa.  
 Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ikiwasili kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo, ndege hiyo imepewa jina la moja ya hifadhi  ya mbuga za wanyama  Ngorongoro kama inavyoonekana kwenye picha. 
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakiwa wamesimama mbeleya  ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuipokea leo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ndege hiyo ni ya kwanza kununuliwa na serikali ya Afrika (Tanzania). 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius  Nyerere, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Ally Bashiru, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel ,na Kulia ni Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)  Mhandisi Ladislaus Matindi, Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa mara baadya ya kuzindua ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyowasiri leo 11 Januari, 2019 kulia ni , Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi mara baada ya mapokezi ya Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyopokelewa uwanja wa Kimataifa Julius Nyerere leo 11 Januari 2019.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...