Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerejea nyumbani baada ya ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.

Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic ChangeNelson Chamisa amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.

Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa watu 12 wameuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitisha.

Jumuia ya Wafanyakazi iliyoitisha maandamano hayo imesema kiongozi wake Japhet Moyo amekamatwa pia.

Hapo jana Mahakama kuu mjini Harare ilitoa uamuzi kuwa waziri wa serikali hana haki ya kuagiza kufungwa kwa mawasiliano ya internet.Huku hali ya wasiwasi ikiongezeka, serikali Jumapili ilisema kuwa hatua za vikosi vya usalama ni 'utangulizi wa mambo yanayotarajia kushuhudiwa'.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...