Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
TAMASHA la 16 la sauti za busara linatarajia kuanza Zanzibar mwezi febuari 7 hadi 10 kwa miondoko ya kiafrika kwa mara nyingine kupitia orodha ya wasanii ambao watanogesha watazamaji kwa aina mbalimbali ya muziki . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema kuna kila sababu ya kusherehekea tukio hilo msimu huo,kutokana na wasanii waliochaguliwa na bei za tiketi.
"Zanzibar itawakaribisha wapenzi wa muziki kutoka katika Kila Kona ya dunia,wakijumuika pamoja kusherehekea upekee wa sauti kutoka nchi ya Algeria hadi Zimbabwe kutoka cape Town hadi Casablanca " alisema Mahmoud. Hata hivyo Mahmoud ameeleza lengo la tamasha hilo ni kuwatangaza wasanii wachanga na wale wanaochipukia kutoka Afrika mashariki.
Pia ametaja bendi kama wamwiduka kutoka Mbeya na Skide kijana anayefanya muziki wa aina ya singeli ambao asili yake halisi ni Tanzania na kwa sasa unakaribia kuuteka ulimwengu. Aidha ametaja lengo la kuwepo tamasha la sauti za busara si tu kwa ajili ya kuburudisha watu bali pia kueleimisha jamii na kuangaza maovu yanayoletwa na rushwa likiwa kama tatizo linaloendelea kuwanyima vijana haki zao za kimsingi na hasa wanamuziki wa kike.
Kwa upande wake Meneja Journey Ramadhan amesema kuwa tamasha la sauti za busara linatangaza Tanzania na Zanzibar na ulimwengu kote kupitia muziki. Ramadhan ameeleza jinsi gani tamasha hilo linawavuta karibu waandaji wa matamasha wa kimataifa ,linawapa fursa wanamuziki wetu kuwasilisha kazi zao kwa hadhira ya kimataifa
"Orodha ya mwaka huu inayo wasanii kama Fid Q, Damian Soul, Mkubwa na Wanawe Crew, Stone Town rockerz, Tausi Women's Taarab, Rajab Suleiman, Kithara, Afrigo band, Jackie Akello na Eli Maliki (Uganda) Fadhilee Itulya na Shamsi Music kutoka Kenya." alisema Ramadhan.
Hata hivyo tamasha la sauti za busara linadhaminiwa na ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswis nchini Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani na Shirika la Ethiopia na Zanzibar Media Corporation.
Mkurugenzi
wa Tamasha la Busara, Yusuf Mahmoud akizungumza na wanahabari leo
jijini Dar es Salaam kuelezea jinsi walivyoweza kujipanga kuwapa
burudani wakazi wa Zanzibar kuanzia Feb 7-10 ndani mji mkongwe. Pembeni
yake ni Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen
(katikati) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tamasha la
Busara Bi. Julia Bishop (kwanza kulia). Picha zote na Cathbert Kajuna -
Kajunason/MMG.
Balozi
wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen akizungumza na
wanahabari jijini Dar es Salaam leo kuelezea machache jinsi walivyoweza
kujipanga kuthamini tamasha la Busara linalotarajia kufanyika Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tamasha la Busara Bi. Julia
Bishop (wa tatu toka kulia) akizungumzia jinsi ambavyo Tamasha hilo
limekuwa msaada mkubwa katika kutangaza utamaduni wa mwafrika. Wengine
ni Mkurugenzi wa Tamasha la Busara, Yusuf Mahmoud (kwanza kushoto),
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen na Meneja wa
Tamasha la Busara Journey Ramadhani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...