Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo wakati akiagiza wavuvi wote waliokamatwa waachiwe huru.

Na.Alex Sonna,Dodoma.

Serikali imeagiza wavuvi wote waliokamatwa kwa kosa la kutohuisha leseni zao za Uvuvi na vyombo vyao kwa mwaka 2019, waachiwe na makosa yao yafutwe mara moja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,wakati akitoa maagizo hayo. Amesema kuwa Wizara yake juzi ilipata tarifa kutoka vyombo vya habari kwamba wavuvi katika ukanda wa Pwani bahari ya hindi hususani soko la feri Dar es saalam, hawakwenda kuvua samaki kwasababu ya kosa la kutokuwa na leseni za vyombo vyao na za uvuvi kwa mwaka 2019.

Kutokana na hali hiyo Ulega aliagiza kuwa wavuvi wote waliokamatwa kwa kosa hilo kote nchini kuachiwa mara moja kuendelea na shughuli zao huku akiwataka maafisa uvuvi kutoka katika ofisi zao na kuwafuata katika mialo mbalimbali ili kuwakatia leseni.

"Kwa kuzingatia kuwa hiki ni kipindi cha mwanzo wa mwaka ambapo leseni zinatolewa Wizara inaelekeza kwamba wavuvi wote waendele kukatiwa leseni hadi Januri 31, 2019"amesisitiza Ulega. Hata hivyo amewaagiza maafisa wote wa Wizara na Halmashauri katika kipindi hiki wawafuate wavuvi kwenye mialo ili kuwakatia leseni wenye sifa kulingana na sheria na kanuni za uvuvi.

Ulega amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inalojukumu la kuhakikisha kuwa rasilimali za uvuvi nchini zinasimamiwa, kuhifadhiwa na kuvunwa kwa kuzingatia sheria ili ziwe endelevu. "Kazi hii inapaswa kufanyika kwa kushirikiana na Halmashauri nchini na wadau wa Uvuvi'alisema Amesisitiza kuwa katika kutekeleza jukumu hilo Wizara imekuwa ikiendesha oparesheni dhidi ya Uvuvi haramu na biashara haramu ya samaki na mazao yake kwa takribani kipindi cha mwaka mzima. 

"Shughuli za uvuvi zinatakiwa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria ya uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na sheria nyingine za nchi... "Kwa kuzingatia hilo kila mtu anayehusika na shughuli za uvuvi anatakiwa kuwa na leseni halali ya uvuvi na na leseni ya chombo anachotumia kwajili ya Uvuvi"alisema Ulega Amesema kuwa Serikali inatoa wito kwa wavuvi wote kuzingatia sheria ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati akiagiza wavuvi wote waliokamatwa waachiwe huru.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo wakati akiagiza wavuvi wote waliokamatwa waachiwe huru.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo wakati akiagiza wavuvi wote waliokamatwa waachiwe huru.Picha Zote na Alex Sonna-Fullshangweblog,Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...