Serikali ya Rwanda imetangaza kupiga marufuku aina yoyote ya matangazo ya biashara ya madawa ya kijadi au asili na kuamuru vyombo vya habari vya nchi hiyo kusitisha vipindi vya waganga wa kijadi kunadi umaarufu wao.

Biashara ya madawa ya kijadi imeshamiri Rwanda na wizara ya afya inasema waganga wengi wa jadi wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kupotosha wananchi.

Kulingana na tangazo la wizara ya afya ya Rwanda ni marufuku kutangaza biashara ya madawa kwa kutumia picha, mabango au pia kutumia vipaaza sauti barabarani kote nchini Rwanda.

Vyombo vya habari pia kama magazeti, mitandao ya kijamii , redio na televisheni vimekatazwa kupitisha vipindi na matangazo yoyote ya biashara kuhusu uganga wa kijadi.

Matangazo au vipindi kuhusu waganga na madawa ya kijadi siku hizi imekuwa biashara kubwa sana kwa karibu vituo vyote vya redio na televisheni za kibinafsi nchini Rwanda.

Waganga wa kijadi wenyewe wakipishana moja kwa moja kila mmoja akitangaza umaarufu wake kutibu magonjwa sugu wanayosema kwamba yamekosa tiba ya kizungu.Wengine wanakwenda mbali na kutangaza kuwa wanatoa madawa ya Baraka na kutibu umaskini huku wengine wakisema wazi kuwa wachawi.Tangazo hilo limezua hisia mbali mbali miongoni mwa waganga wa jadi.

Baadhi wamesikitishwa na uamuzi wa wizara ya afya wa kuwakataza kutangaza biashara yao kupitia vipindi vya redio:

''Sijafurahishwa na uamuzi huu kwa sababu ingekuwa vizuri wizara ya afya kwanza ikatuuliza ukweli wa yale tunayozungumzia, halikadhalika ubora na uhalali wa madawa tunayotumia.

Mimi nilikuwa nafanya matangazo mengi ya biashara yangu kupitia vyombo vya habari ili watu wafahamu umaarufu wangu wa kutibu magonjwa, ila ninachosema kama kuna mmoja wetu aliyefanya kosa la kusema kwamba anafanya miujiza, sote hatuwezi kuathirika kutokana na yeye.'' amesema mmoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...