Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Shirika la bima Zanzibar limedhamini mashindano ya riadha ya Mererani Tanzanite Half Marathon ambayo yatafanyika mwishoni mwa wiki na kujumuisha idadi kubwa ya wanariadha kutoka mikoa ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa shirika la bima Zanzibar kanda ya Kaskazini Hamis Matumla alisema hayo Jana wakati akikabidhi kiasi cha shillingi milioni mbili ambazo ni udhamini was shirika hilo ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono michezo na kuhamasisha umuhimu wa afya kwa wachezaji.
Matumla alisema kuwa kuelekea Mashindano ya Riadha ya Mbio fupi yajulikanayo kama Mererani Tanzanite Half Marathon yatakayofanyika huko Mkoani Manyara ,Wadau wa Michezo wanapaswa kujitokeza kushiriki pamoja na kudhamni Mashindano hayo yenye lengo la kutangaza madini hayo yanayopatikana Tanzania Pekee.

"Jamii inatapaswa kujenga utamaduni wa kupenda kushiriki Michezo kwani michezo ni ajira na michezo ni afya pia" Alisema Matumala

Kwa upande wao waandaaji wa Mashindano hayo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Charles Mnyalu wanasema uandikishaji unaendelea katika Vituo mbalimbali vilivyopo hapa nchini na Washiriki na Washindi watapata Zawadi Mbalimbali.

Alisema Mbio hizo zitakazofanyika mnamo tarehe 27 mwezi huu katika Viunga vya mji wa Mererrani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara zitashirikisha wanariadha wa kilometa tano ambao ni Watoto pamoja na Kilometa ishirini na Moja kwa Watu Wazima huku zaidi wanariadha elfu moja mia tano wakitarajia kushiriki.

Mjumbe Kamati ya Mashindano Alfredo Shahanga aliwataka Wakazi wa manyara ,Arusha na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...