Na Bakari Madjeshi,  Globu y'all Jamii
Wakati Michuano ya Sportpesa Cup 2019 yakitarajiwa kuanza hapo kesho, Januari 22, Mkurugenzi wa Udhibiti na Utawala wa Sportpesa Tanzania,  Abbas Tarimba amezitaka timu za Tanzania zinazoshiriki Michuano hiyo kuacha mzaha kwa kuingiza uwanjani time za vikosi vya pili

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Tarimba amesema kuwa anapenda kuona Taji la Michuano hiyo kwa mwaka huu linabaki hapa nchini kutokana na tayari Kenya kulibeba mara mbili mfululizo. 

"Nimekutana na Viongozi wa timu zote mbili za Simba na Yanga zimeongea nao kuelekea kwenye Michuano hii, niwewaambia waache mzaha safari hii, kuna zawadi nono tusingependa ziondoke tena Kenya", amesema Tarimba. 

Katika Michuano hiyo itakayoshirikisha timu Nane kutoka Kenya na Tanzania itaanza kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar huku timu za Singida United na Young Africans zitarajiwa kutupa karata zao. Yanga SC itamenyana na Kariobangi Sharks majira ya saa 10 za jioni wakati Singida United ikichuana na Bandari majira ya Saa 8 mchana kwenye dimba hilo hilo la Uwanja wa Taifa.

Kuelekea kipute hiko cha ufunguzi majira ya saa 10, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa wamejiaanda vizuri kushiriki Michuano hiyo, ambapo amesema kuwa watajitahidi kuwaangalia wapinzani wao (Kariobangi Sharks) ili kuwajua zaidi ili kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Naye Nahodha wa Kikosi hicho, Ibrahim Migomba amesema kuwa watajitahidi kufanya vizuri kwenye Michuano hiyo kutokana name maandalizi walionayo kuelekea mchezo wao dhidi ya Kariobangi Sharks, Ajib amesema kuwa kuna siri wamepewa na Kocha wao Mwinyi Zahera hivyo kuna uwezekano wakupata ushindi mzuri dhidi ya timu hiyo ya Kenya.
Mkurugenzi wa Udhibiti na Utawala wa Sportpesa Tanzania, Abbbas Tarimba akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuelekea Michuano ya Sportpesa Cup 2019 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Kesho, Januari 22.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...