Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa Timu ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa kwanza katika Kundi D baada ya kuifunga JS Saoura goli 3-0.

Simba wakiwa wako katika uwanja wa nyumbani wa Taifa walianza kwa kasi kulisakama lango la JS Saoura na ilichukua dakika 45 kwa Mshambuliaji Emanuel Okwi kuandika bao la kuongoza kwa shuti kali baada ya ‘kuwapinduapindua’ mabeki wa JS Saoura kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.

Okwi aliyekuwa katika kiwango cha juu leo, alifunga bao hilo akitoka kukosa bao la wazi baada ya kugongesha nguzo ya juu akiwa tayari amemtoka beki anatazamana na kipa.    

Simba Walifanya mabadiliko dakika ya 34 wakimtoa Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kuumia nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mwenzake, Meddie Ksgere kutoka Rwanda. 

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kurudi na nguvu mpya na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yote yakifungwa na Kagere Goli la pili akifunga dakika ya 51 akimalizia pasi ya Okwi ambaye mabeki wa JS Saoura na lingine akifunga tena dakika ya 67 kwa mara nyingine akimalizia pasi nzuri ya Okwi.

Nahodha wa Simba John Bocco amesema mwitikio wa mashabiki Uwanjani umewapa morali kubwa hali iliyowafanya wapate nguvu na kushinda  mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura.

Bocco amesema mashabiki wanaumuhimu na nguvu kubwa wakiwa Uwanjani anafurahi kuwaona namna wanavyokuwa begakwabega na timu yao."Tunachoangalia sisi ni pointi tatu bila kujali nani anafunga na nani anakosa, makosa yapo na kwenye mpira mengi yanatokea ila sapoti ya mashabiki inatupa nguvu ya kupambana," alisema Bocco.

Mechi nyingine ya Kundi D inachezwa  Saa 4:00 usiku wa leo Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria kati ya wenyeji, Al Ahly dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Baada ya mchezo wa leo, Simba SC itasafiri kuwafuata AS Vita mjini Kinshasa Januari 19, wakati JS Saoura watakuwa wenyeji wa Ahly Januari 18 nchini Algeria.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Hassan Dilunga/Muzamil Yassin dk65, Jonas Mkude, John Bocco/Meddie Kagere dk37, Emmanuel Okwi/Shiza Kichuya dk86 na Clatous Chama.
 Moja ya heka heka iliyotokea kwenye lango la JS Saoura wakati Kipa wa timu hiyo, Khaled Boukacem akichuana  na Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi wakati akijaribu kutafuta namna kukwamisha mpira wavuni. 
 Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akishangilia moja ya bao alililofunga kwenye mchezo wa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Simba iliondoka na ushindi wa bao 3-0
 Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akishangilia moja ya bao alililofunga kwenye mchezo wa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Simba iliondoka na ushindi wa bao 3-0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia mtanange huo baina ya Simba SC dhidi ya JS Saoura ya Algeria, mchezo uliomalizika jioni hii katika Uwanja wa Taifa.
 
 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...