WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), imewajengea uwezo na kuwapa mbinu za kutafuta ajira pindi wanapomaliza masomo zaidi ya wanafunzi 500 wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Huduma zinazotolewa na TaESA ni kuunganisha watafuta kazi na waajiri, kutoa mafunzo kuhusu mbinu za usaili ambayo huwajengea uwezo wa kujiamini, kutoa ushauri kuhusu masuala ya ajira na kutoa taarifa za soko la ajira.

Akizungumza mjini Arusha Afisa Kazi Mwandamizi wa TaESA na Mratibu wa Mafunzo hayo kwa wanafunzi Peter Ugata alisema, Tanzania na dunia kwa sasa kuna changamoto zinazohusiana na Soko la Ajira. Alisema hatua hiyo imechangiwa na mahitaji ya Waajiri kuhamia kwa watu wenye ujuzi wa ziada mbali ya na weledi wa kusomea, kwani mara nyingi ujuzi wa ziada hausomewi.

“Changamoto zilizopo zimeletwa na mabadiliko ya dunia ya utanfawazi ambapo watu, huduma na bidhaa ziko huru kutoka sehemu moja hadi nyingine. “Ili kukabiliana na hali hiyo nchi mbalimbali duniani zilianzisha huduma za Ajira kupitia Sera, Sheria, Kanuni na maazimio ya Shirika la Kazi Duniani (ILO),” alisema.

Akifafanua namna huduma za ajira zinavyotolewa Ugata alisema Wakala husajili na kutunza taarifa za watafuta kazi kwa kutumia Kanzidata iliyopo. “Wakala huoanisha sifa za mtafuta kazi kulingana na mahitaji ya kazi husika kama yalivyoanishiwa na mwajiri, lakini pia wakala unaoanisha ujuzi, uzoefu, elimu na sifa nyingine za watafuta kazi na mahitaji ya sifa za kazi za mwajiri,” alisema Ugata.

Anazitaja baadhi ya faida za kutumia TaESA ni Waajiri kupewa ushauri mzuri kuhusu mwenendo wa soko la Ajira na mahitaji na aina ya watu na ujuzi utaokamsaidia kuleta tija. “TaESA itamuwezesha mwajiri kupata wafanyakazi kazi waadilifu na waaminifu katika kazi, wabunifu na wakujituma kazini , lakini pia kuiwezesha serikali kupata takwimu za uamuzi na mipango kwa haraka,” alisema Ugata.

TaESA inafanya kazi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu. 
Afisa Kazi kutoka TaESA Emma Mangesho akiwajengea uwezo na kuwapa mbinu Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kuhusu namna bora ya kutafuta kazi 
Meneja wa Karakana ya uchomeleaji Chuo cha Ufundi Arusha Expedito Miliaso akiwaonyesha maofisa wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), vifaa vipya vya uchomeleaji wanavyotumia wanafunzi wa Chuo hicho kwa ajili ya mafunzo. 
Maofisa wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) kutoka Dar es Salaam na Arusha wakiangalia kifaa maalumu cha uchomeleaji ndani ya Karakana ya Chuo cha Ufundi Arusha anayewaonyesha ni Meneja wa Karakana ya uchomeleaji Expedito Miliaso. 
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakimsikiliza Afisa Kazi wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESO) kutoka Dar es Salaam Emma Mangesho akifundisha namba bora ya uandishi wa barua za kuomba ajira.
Afisa Kazi wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESO) kutoka Dar es Salaam Emma Mangesho akifundisha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), mbinu za kuomba ajira ikiwamo namna bora ya uandishi wa barua za kuomba kazi. 
Afisa Kazi Mwandamizi kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) na Mratibu wa mafunzi Peter Ugata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wakati wa kuwajengea uwezo wa namna bora ya kutafuta kazi.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...