Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

JITIHADA za Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) Mkoa Arusha la kuhakikisha kunakuwa na nishati ya umeme ya kutosha na ya uhakika imeongeza chachu cha kuvutia wawekezaji huku Meneje wa shirika hilo ndani ya mkoa huo Mhandisi Herini Mhina akitoa rai kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi waende kuwekeza.

Pamojana jitihada hizo za kuimarisha upatikanaji wa umeme , TANESCO mkoa wa Arusha inajivua ziada ya umeme iliyopo ambapo kwa sasa wanazalisha megawati 120 lakini mahitaji ya umeme kwa mkoa ni megawati 75, hivyo hawana tatizo la upungufu wa nishati hiyo.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini waliopo katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya umeme ambayo inatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya kiongozi mahiri Rais Dk.John Magufuli kupitia Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi Mhina amesema shirika hilo linajivunia mafanikio makubwa katika sekta hiyo na kwa Mkoa wa Arusha umepiga hatua zaidi.

"TANESCO Mkoa wa Arusha tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha sekta ya umeme nchini.Tumefanikiwa kuongeza uzalishaji na hivyo kwetu hapa tunayo ziada ya umeme kwani tunayozalisha ni megawati 120 lakini mahitaji yetu kwa sasa ni megawati 75.Tumeendelea kusambaza umeme kwa wateja wetu wakubwa, wakati na wadogo,"amesema Mhandisi Mhina huku akisisitiza mkakati wao wa kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme inakwenda sambamba na kauli mbiu ya utekelezaji wa Tanzania ya viwanda.

Amefafanua kutokana na kuwa na umeme wa uhakika, hivyo TANESCO Mkoa wa Arusha linaendelea kuhamasisha wawekezaji kuwekeza ndani ya mkoa huo kwa kujenga viwanda ambavyo faida yake ni kubwa kwa Taifa na kusisitiza tayari wapo wawekezaji ambao wamewekeza na faida yake inaonekana.

Kuhusu miradi ya umeme inayoendelea , Mhandisi Mhina amesema kuna utekelezaji wa miradi ambayo ipo ambayo tayari imekamilika na hivyo kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wateja wakati miradi mingine ipo hatua mbalimbaliza utekelezaji wake.
 
Amesema kukamilika kwa miradi hiyo ya TANESCO Mkoa wa Arusha, imekuwa chachu hata ya kufanya vijana wengi ndani ya mkoa huo kupata fursa ya kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo"Kutokana na uwepo wa umeme wa uhakika wananchi wengi na hasa vijana wamejiajiri kwa kuanzisha viwanda hivyo vidogo vikiwamo vya utengenezaji matofali."
 
Kuhusu changamoto, Mhandisi Mhina amejibu kuwa hawana tatizo la kukatika kwa umeme na iwapo utakatika ni kwasababu maalumu ya matengenezo ya miundombinu na kabla ya kuukata wanatoa taarifa mapema kwa wananchi.Hata hivyo ameeleza changamoto iliyopo ni baadhi ya wananchi kupanda miti kwenye njia za umeme na hivyo wakati mwingine kusababisha hasara kwani nyaya nyingi hazina ngozi , hivyo mti unapoangia husababisha madhara. "Hivyo tumekuwa tukiwahamasisha wananchi kukata miti kwenye njia ambazo umeme unapita na sisi wenyewe tumekuwa tukifanya usafi wa mara kwa mara,"amesema.

Wakati huo huo ameeleza ambavyo wamefanikiwa kuondoa tatizo la umeme mdogo ambao ulikuwa kero kwa wateja wao kwani hivi sasa umeme uliopo ni mkubwa ambao umeondoa malalamiko yaliyokuwepo siku za nyuma.
Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina(kushoto), akimsikiliza Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani, Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua kuhusu namna TANESCO ilivyoweza kufikisha umeme wa kutosha kwenye eneo la Mirarani leo Januari 21, 2019.
Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina
Kituo cha kupokea umeme kilichoko ndani ya kiwanda cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe, (graphite) huko Mirerani mkoani Manyara ambapo TANESCO imefu nga mitambo na transfoma kubwa tatu ili kutoa umeme toshelezi kwa kiwanda hicho.transfoma pozo kubwa tatu zilizofungwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...