Katika kuhakikisha jamii ya Kitanzania inafanikiwa na kufaidika kwa uwepo wake kampuni ya simu nchini Tanzania TECNO Mobile yahakikisha zaidi ya watoto 100 ambao ni yatima wanapata vifaa vya shule. 

TECNO imefanikiwa kuchangia fedha pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa kituo cha Chanika Children Shelter kinacholea watoto yatima kilichopo chanika, jijini Dar es salaam, katika kituo hicho takribani watoto wenye umri tofauti kuanzia miaka 4 mpaka 18 wanalelewa kwa usaidizi mkubwa wa mmiliki wa kituo hiko kiongozi wa madhehebu ya budha nchini Dr. Pannasekara.
Akizungumza wakati wa makabidhiano meneja wa uhusiano wa kampuni ya simu ya TECNO bwana Erick Mkomoye alisema kwamba, “ndoto za Watoto hao ndio zilizopelekea kampuni ya simu ya TECNO kuanzisha kampeni inayofamika KUWA SHUJAA WANGU na kuanzia kwa kuchangia hundi ya kiasi cha millioni 5 ili kutimiza mahitaji yao ya shule, tuliwashawishi watanzania na wateja wetu kuwasaidia watoto hawa kadri wawezavyo lakini pia sisi kama kampuni pia tutawasaidia watoto hawa kuhakikisha ndoto zao zinatimia tumeanza na million 5 na tutaendelea. ”

Bwana Eric aliongeza, “KUWA SHUJAA WANGU ni kampeni ambayo imepelekea kuwasaidia watoto wa Chanika Children Shelter ili kutimiza ndoto zao za kwenda shule na kuanza masomo yao katika ngazi tofauti tofauti sekondari na msingi na hata chekechea ili baadae waje timizia ndoto kubwa zaidi za kuwa daktari, mwalimu, rubani katika kulifanikisha hili TECNO tumeamua kuipa muendelezo kampeni hii kwa mwaka wote huu wa 2019”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...