BENKI ya NMB imesema inatambua umuhimu wa elimu na afya kwa Watanzania hivyo itaendelea kusaidia katika sekta hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za Serikali za kuwahudumia wananchi wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Benki hiyo, Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola wakati akikabidhi msaada wa madawati 102 kwa shule za Msingi Mwasanga na Hekima za Jijini Mbeya.

Pia Benki ya NMB imekabidhi jumla ya mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli ya Wilaya Mbeya na Mapinduzi ya Jijini Mbeya na vitanda, magodoro na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi vyote vikiwa na thamani ya milioni Sh25. Alisema NMB ni wadau muhimu kwa Serikali na Watanzania hivyo wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa sababu jamii wanayoisaidia ndiyo inayowawezesha kupata faida katika biashara yao.

“Tunambatua changamoto ya elimu na afya, sisi NMB tunazipa kipaumbele sana kwa sababu hizi sekta mbili ni muhimu mno katika ustawi wa jamii yetu,” alisema Chilongola.Chilongola alisema katika kipindi cha mwaka huu wa 2019, NMB imetenga Sh1 bilioni kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwamo afya, elimu na yanapotokea majanga kwa nchi nzima.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Mwasanga, Keneth Amon alisema shule yake inakabiliwa na msongamano wa mkubwa wa wanafunzi madarasani kutokana uhabawa wa vyumba vya madarasa, upungufu wa madawati.Alisema ‘Msongamano ni mkubwa sana darasani, shule nzima tuna madawati 237 lakini kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi, tunakabiliwa na upungufu wa madawati 140, lakini vile vile tuna upungufu wa ofisi za walimu. Shule ina walimu 22 na wote tunatumia ofisi moja ambayo nayo ni finyu mno jambo ambalo kwa kweli inatuwia vigumu kumudu majukumu ya kila siku’.

Akizungumza na baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika alisema Benki ya NMB inatambua umuhimu wa kusaidia jamii kama walivyo fanya ikitambua kwamba Serikali pekee haiwezi kufanya kila jambo kwa wananchi wake licha ya kuwa ndio wajibu wake.

Alisema ‘Niwatake wazazi kwamba shule zimeshafunguliwa sasa hivyo asiwepo mwanafunzi ambaye hafiki shuleni, na nyinyi wanafunzi hakikisheni mnatunza madawati haya na msome kwa bidii. Leo NMB imetambua umuhimu wa elimu bora kwa kuwatengenezea mazingira bora ya kusomea na ndiyo maana imeleta madawatin haya’.

Ntinika amefafanua kuwa mahitaji ya huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu yanahitaji kuungwa mkono na taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii kama ilivyofanywa na Benki ya NMB ambayo imechangia vitanda na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya - William Pauk Ntinika akipokea Msaada wa madawati 51 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu - Straton Chilongola kwa ajili ya shule ya Msingi Mwasanga Jijini Mbeya. Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akipokea mashuka kwa ajili ya Hospitali Teule ya Ifisi ya jijini Mbeya kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu - Straton Chilongola. Kwa ujumla, Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika mabati 144 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Mapinduzi Jijini Mbeya. Kwa ujumla, Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25. 


Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwasanga wakiwa wameketi kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB baada ya makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo. Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...