Martin Fayulu amedai kuwa mshindi ameteuliwa na utawala wa Kabila ili akidhi matakwa yao


Mgombea wa upinzani aliyeshindwa katika uchaguzi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) uliofanyika Disemba 30 ameapa kuyapinga matokeo mahakamani.

Martin Fayulu ameiambia BBC kuwa raia wa Congo wanastahili kujua ukweli wa uchaguzi, mabao ameutaja kuwa ni "mapinduzi".

Mgombea mwengine wa upinzani Felix Tshisekedi, alitangazwa kuibuka na ushindi katika kinyang'anyiro hicho, lakini kumekuwa na tuhuma kuwa mshindi huyo ameingia makubaliano ya kisiasa na rais aondokaye Joseph Kabila.

Tayari watu kadha wanaripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa toka matokeo hayo yalipotangazwa.Uchaguzi huo unakamilisha safari ya miaka 18 madarakani ya Joseph Kabila.

Matokeo hayo, endapo yatathibitishwa, yataweka historia ya makabidhiano ya amani ya hatamu za uongozi toka nchi hiyo ilipopata uhuru wake toka kwa wakoloni wa Ubelgiji mwaka 1960.

Kanisa lenye ushawishi mkubwa la Katoliki ambalo lilikuwa na waangalizi wa uchaguzi 40,000 limesema matokeo yaliyotangazwa hayaendani na matokeo waliyonayo.

Fayulu amesema nini?

Akiongea na mhariri wa BBC wa Afrika Fergal Keane, Bw Fayulu amesema atayapinga matokeo hayo kwenye mahakama ya katiba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...