Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHANGWE,nderemo na vifijo vimetawala katika Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam wakati wa Watanzania zaidi ya milioni 50 wakiangalia angani wakisubiri kuipokea ndege mpya ya Airbus 220-300 inayowasili leo mchana huu.

Mamia ya wananchi wamejitokeza kwa ajili ya kushuhudia ujio wa ndege hiyo ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo mawaziri wamewasili uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa ratiba ambayo imetolewa kuhusu ujio wa ndege hiyo inaeleza kuwa  Rais Dk.John Magufuli atawasili uwanjani hapo saa nane kamili mchana.Na kabla ya hapo atawasili Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Baada ya viongozi hao kuwasili utaimbwa wimbo wa Taifa na kisha itafuata dua kutoka kwa viongozi wa dini  .Kwa mujibu wa ratiba itafuata hatua ya kutambulisha viongozi wa ngazi mbalimbali.

Itakapofika saa 8:30 hadi 8:40 ndege itawasili na kisha kupokea water Salute na baadae itafuata taarifa ya ndege.Saa 8:50 hadi 9:00 ndege itazinduliwa na baada ya hapo yatafanyika makabidhiano.

Kutakuwa na maelezo ya Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ambaye atamkaribisha mgeni rasmi .Saa 9:20 Rais Magufuli atazungumza na watanzania kupitia hotuba yake atakayoitoa uwanjani.

Mtanzania angalia angani...Endelea kufuatilia Michuzi Blog na Michuzi Tv kwa taarifa mbalimbali zinazoendelea kuhusu ujio wa ndege hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...