Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MSANII wa vichekesho nchini aliyejizolea umaarufu kutokana na umahiri na uhodari wa kuchekesha Yusuph Kaimu 

a.k.a Pembe ametoa ujumbe kwa wasanii na waigizaji wa vichekesho ambao ni chipukizi kuwa wabunifu katika kazi zao kwa lengo la kuteka soko la sanaa hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki.

Pembe ametoa kauli hiyo leo Januari 17, 2019 wakati anazungumza na Michuzi Blog ambapo amefafanua kwa sasa wasanii wengi wa vichekesho wanafanya kazi kwa kuigana na hivyo kuwa ngumu kumtambua msanii kutokana na sauti anayotumia inatumiwa na wasanii wengi.

"Wasanii wengi wanatumia sauti ya aina moja wakati wa kuigiza na hivyo kuwa ngumu kutambua anayechekesha kwa wakati husika.Hivyo ni vema wakabadilika na kuwa wabunifu kwa kila mmoja kuwa na sauti yake na staili yake ambayo itakuwa rahisi kutambua,"amesema Pembe.

Akizungumzia utofauti wa tasnia ya filamu kwa miaka ya zamani na sasa, Pembe amesema hapo nyuma wasanii walishandana na kuonesha vipaji vyao halisi vya kuigiza na kuchekesha na kwamba walikuwa na nidhamu ya 
kazi."Umahiri wa waigizaji wa zamani ulisababisha hata kufanya uwepo ushawishi uliosaidia kuvuta wadau wengi kuwa karibu na tasnia hiyo,"

Amewataja baadhi ya wasanii wa vichekesho ambao wamejizolea umaarufu kutokana na umahiri wao ni Senga,Bambo na Kingwendu ni wasanii ambao wamekuwa maarufu kutokana aina ya lafudhi zao za sauti zao ambazo 
walikuwa wanazitumia kwenye kuigiza na kwamba unaposikia sauti unajua tu huyo ni Bambo au huyo ni Kingwendu ama Senga.

Amesisitiza kupitia lafudhi zao wasanii hao wamekuwa mfano tosha na mpaka sasa wamebaki kwenye aina ya uwasilishaji wao wa sanaa huku akieleza kuwa hata pale ambapo watu wanapewa tuzo n vema kukawa na utaratibu wa kutambua waliofikisha sanaa hiyo hapo ilipofika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...