Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
Katika shambulio lililotekelezwa na kundi la kigaidi la wanamgambo wa Alshabab hapo jana katika  eneo la Riverside mwandishi wa habari aliyekuwa akiandika habari za michezo katika blogu ya Wadau TV na shabiki wa soka nchini humo  James Oduor maarufu kama Odu Cobra ameuwawa katika shambulio hilo siku moja kabla ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa.

Odu alishiriki wakati wake wa mwisho na mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa twitter kwa kuchapisha kile kilichokuwa kinaendelea baada ya kuwa mateka ila Mungu alimpenda zaidi na alifariki kabla ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa leo Januari 16.
Shambulio hilo lilitekelezwa jana na kundi la wanamgambo wa Alshabab  majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Riverside ambako hoteli ya DusitD2 na ofisi za makampuni mbalimbali zinapatikana.

Chanzo: The StandardMedia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...