Na. Vero Ignatus,Arusha


Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuwa wabunifu kwa kubuni bidhaa zinazoweza kuhimili ushindani katika soko la pamoja la Afrika Mashariki ili waweze kunufaika na fursa za uwepo wa soko hilo pamoja na kuboresha maisha yao.


Hayo yanesemwa na Wawakilishi wa vijana kutoka Majukwaa ya vijana Wilaya ya Arusha katika Mafunzo ya Ujasiriamali yanayolenga kukuza ubunifu na uwezo wa vijana kutumia fursa za kimasoko kujikwamua kiuchumi .

Farida Charles na Denis George walisema kuwa ,vijana wengi wamekuwa wakijitahidi kubuni bidhaa zao lakini changamoto kubwa bado ipo katika ubora wa hizo bidhaa katika kushindana na soko la Afrika Mashariki.

Kutokana na changamoto hiyo vijana hao kwa pamoja walijiwekea mikakati ya kuhakikisha kuwa bidhaa zote wanazozalisha ni lazima ziendane na soko la Eac ili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo na kupata masoko zaidi.

Mratibu wa shirika la Vijana la Initiative for Youth ,Laurent Sabuni alisema kuwa, vijana wa kitanzania hawapaswi kuwa nyuma katika soko la pamoja la Afrika Mashariki kwani wanapaswa kuungana na kufanya biashara kwa kuvuka mipaka ya nchi na kuzalisha bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Sabuni alisema kuwa, kumekuwepo na fursa nyingi Sana katika soko la jumuiya ya Afrika mashariki ambazo vijana wanatakiwa kuzichangamkia na kuondokana na dhana ya kulia ukosefu wa ajira, badala yake wajikite katika kuzalisha bidhaa zitakazoendana na soko hilo.

Afisa Vijana Wilaya ya Arusha, Nimfa Ramadhani alisema kuwa ,Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa viwanda, hivyo vijana wana fursa ya kutengeneza bidhaa za viwandani na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kuendana na kasi ya ujenzi wa viwanda iliyopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...