Na Sylvester Raphael,Kagera

VIONGOZI  wa madhehebu ya dini Mkoani Kagera wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais DkJohn Magufuli kwa kuchukua hatua na maamuzi yanayolenga kumuinua mwananchi mnyonge ili afaidike na raslimali za nchi yake.

Wametoa pongezi hizo jana Januari 16,2019 baada ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ofisini kwake kwa mazungumzo.

Hivyo wametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini na yenye manufaa kwa umma mfano ununuzi wa ndege, ujenzi wa Reli ya Kisasa na ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge pamoja na miradi mingine mingi ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza kwa niaba yao Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini amesema pia wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kudumisha amani, utulivu na mshikamano kwa Watanzania na kuendelea kutekeleza shughuli ambazo zinalenga maslahi mapana ya wananchi.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wa madhehebu ya dini walimweleza Mkuu wa Mkoa Gaguti kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali ya mkoa katika kudumisha amani na utulivu katika mkoa huo.

 Pia wameahidi wataendelea kuhamasisha wananchi kuchapa kazi kwa bidii kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa kama jina la mwaka 2019 kwa lugha ya Kihaya linavyohimiza kila mwananchi kufanya kazi likimaniisha kuwa kila mmoja atakula kwa jasho lake “Biluga Omumpiita”.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Gaguti katika mazungumzo hayo aliwahakikishia viongozi hao wa dini kuwa yeye binafsi pamoja na Serikali ya Mkoa wataendelea kushirikiana nao kwani wao ndiyo nguzo kuu ya amani katika mkoa.Pia viongozi wa dini ndio nguzo kuu ya maadili hasa kwa kuiunganisha Serikali na wananchi wake.

“Serikali tutaendelea kushirikiana na nyinyi kama ilivyo desturi ya Mkoa wetu wa Kagera na tunawategemea sana katika kuhakikisha mkoa wetu unaendelea kudumisha amani na utulivu kwani kila mara mnapokutana na waamini wenu mkahubiri kuhusu amani na utulivu sisi kwetu kazi inakuwa ndogo. 

"Pia mnapowahimiza wananchi wafanye kazi kwetu sisi Serikali inakuwa rahisi mno kuweka msukumo kwa wananchi," amesema Gaguti

Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Viongozi wa Madhehebu ya Dini waliokuwepo ni ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoriki la Bukoba Kilaini, Sheikh Aruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera na Askofu Dk. Abedinergo Keshomshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania Dayosisi ya Kasikazini Magharibi.
Askofu Msaidizi Jimbo Katoriki la Bukoba akizungumza jambo mbele yaMkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti,huku Askofu DKt. Keshomshahara (KKKT) na Sheikh Aruna Kichwabuta wakimsikiliza.
Askofu Msaidizi Method Kilaini na Askofu Dkt. Keshomshahara Wakisikiliza na Kufurahia Jambo Kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti (hayupo Pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti (Kushoto) akimsikiliza Askofu Method Kilaini kwa Umakini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti (Kushoto) Akimsikiliza Sheikh Aruna Kichwabuta (Kulia) Askofu Method Kilaini na Askofu Dkt. Abednergo Keshomshahara wakisikiliza.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti akitoa neno kwa Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoani Kagera
Picha ya Pamoja Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa
Sheikh Aruna Kichwabuta (Kulia) Kwa niaba ya Wenzake akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti Mwongozo wa Namna Viongozi Madhehebu ya Dini Wanavyoshirikiana Mkoani Kagera
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...