WAKULIMA wa kijiji cha Kapunga kilichopo wilaya ya Mbarali mkoani mbeya wameiomba Serikali kuingilia kati kuwaondoa kwa nguvu wavamizi wa mashamba yao na maeneo ya kijiji chao kinyume cha sheria.

Wamesemaa kuwa mashamba hayo ambayo wanayamiliki kiharali yamevamiwa na taasisi inayotambuliwa kama umoja wa wakristo Tanzania UWATA kinyume na taratibu na kusababisha uwepo mgogoro kati yao na wananchi wa kijiji cha kapunga.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii jana wilayani humo kwaniaba ya wenzake mmoja wa wahanga wa mashamba hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Mapogolo Kapunga Sekelaga Sandube alisema kuna umuhimu wa serikali kuu kuingilia kati kwani serikali ya mkoa na wilaya pamoja na juhudi kadhaa kuchukuwa lakini imeshindikana wavamizi kuondoka.

Amesema awali baada ya wavamizi hao kuingia walilipoti ofisi ya kijiji cha kapunga na baadae wilayani ambapo kote huko viongozi mbali na kushughulikia tatizo hilo lakini wameshindwa kuwaondoa wavamizi hao hali iliyosababisha wao kushindwa kuendelea na kilimo katika maeneo hao.

"Ndugu Mwandishi mgogoro umechukua miaka zaidi ya 10 na tumehangaika katika ofisi zote za serikali kwa maana kijiji hadi mkoa na mbaya tumefika hadi kwa Waziri mwenye dhamana na ardhi na kutoa maagizo kwa maandishi ya kuelekeza kuondolewa kwa wavamizi hao mara moja lakini viongozi wa wilaya wameshindwa kutekeleza agizo hilo hadi sasa. "alisema Sandube

Nakuongeza kuwa kutokana na viongozi kushindwa kutekeleza maagizo ya waziri na ofisi ya serikali ya mkoa ndio maana tunaiomba serikali kuu hususani mh Rais Dkt John Magufuli kumaliza mgogoro huo.

Akizungumzia chanzo cha uvamizi wa maeneo hayo Sandube amesema kwa makusudi huku wakiwa wanajuwa wanachokifanya ni kinyume cha sheria ardhi ya vijiji sura 114 ya 2002 uongozi wa serikali ya kijiji cha Ukwavila uligawa maeneo ya kijiji cha kapunga na kusababisha migogoro inayoendelea hadi sasa.

Naye Katibu wa umoja wa kilimo cha umwagiliaji Mpunga mmoja (SKIMU) Emmanuel Mwansanga Alisema mgogoro huo umewsatori kutokana na miundombinu kuharibiwa zikiwemo mbegu ambazo zilikuwa zimepandwa kwa ajili ya maandalizi ya kilimo cha msimu huu.

" Jumla ya hekari 62 ambazo ni mali ya sisi kama wakulima na zaidi ya heri 600 ambazo ndani yake zilitakiwa zigawiwe kwa vijana wa kijiji. nazo zimevamiwa."Amesema Mwansanga

Aliongeza kuwa hekari hizo 600 zilitengwa kutona na maagizo ya Rais Dkt Magufuli aliyoyatoa mwaka 2016 kupitia Waziri William Lukuvi nakwamba nazo zimevamiwa huku viongozi wakishndwa kusimamia maagizo yaliyotolewa.

Kwaupande wake Mtendaji wa kijiji cha Kapunga Jackson Mbilinyi alikiri kuwepo kwa uvamizi huo na migogoro ya ardhi nakwamba wao kama viongozi walijaribu kushughulikia tatizo.

Kwaupande wake Daimon Simwandiya ambaye anadaiwa ni mmoja wa wavamizi wa mashamba hayo akizungumza kwa njia ya simu alisema wao waliyapata maeneo hayo kihalali mwaka 2002 na wakapewa hati ya kimila 2013.

Alipoulizwa kwanini Serikali ya kijjji cha Ukwavila ikawape mashamba kwenye kijiji cha Kapunga amesema wao ni watanzania wanahaki ya kulima popote hata Dar es Salaam wanaweza wakalima.

Naye mkuu wa Wilaya ya Mbarali akizungumzia sakata hilo alisema hana taarifa mgogoro wa uvamizi na kama hao watu waende ofisni kwake.

"Mimi sina taarifa hiii kwamba kuna mgogoro na anachofahamu yeye kwamba kulikuwa na mgogoro wa mpaka ambao mkuu wa mkoa wa mbeya alishaumaliza "amesema Mkuu huyo wa wilaya.
 
Mwenyekiti wa CCM tawi la Mapogolo Kapunga Sekelaga Sandube  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...