Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota ametoa siku 14 kwa wananchi wote waliovamia hifadhi  ya pori la akiba la Swagaswaga kuondoka ndani ya hifadhi kabla ya kuondolewa kwa nguvu. Ameyasema hayo alipokuwa akiongea katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya ili iliyofanyika katika maeneo hayo.

Aliongeza kuwa serikali inayafanya hayo ili kuendelea kuhifadhi rasilimali muhimu zilizomo ndani ya hifadhi hiyo ili ziongezeke na kuongeza idadi ya watalii ambao watakuja kwa wingi kupumzika ndani ya hifadhi baada viongozi mbalimbali kuhamia Dodoma. “Ni wakati maalum sasa watu waheshimu mipaka ya hifadhi na wasikae ndani ya hifadhi sababu serikali ina mkakati  wake madhubuti wa kuendeleza hifadhi zote kama sehemu ya kuongeza pato la nchi”.Alisema Makota

Aliongeza kuwa kaya zote zilizomo ndani ya hifadhi na zinafahamika hivyo ni wakati muafaka kwa wao kuondoka  na kuacha kulima kwa mwaka huu kwani wapo waliokata misitu na kuandaa mashamba. “Pia kwasasa serikali imefanya utaratibu wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya wananchi wanaopakana na hifadhi ambapo kwa sasa wapo katika vijiji vinavyopakana na Tarangire ambapo pia ipo katika wilaya ya Kondoa lengo likiwa ni kuweka matumizi ya kila ardhi husika.”Alifafanua Sezaria

Aidha akiuliza kwa niaba ya wananchi wengine Bwana Hassan Juma alitaka kujua wananchi walio ndani ya hifadhi na walishafanyiwa tathmini watalipwa lini sababu wameshaambiwa wahame?Akijibu meneja wa pori la Swagaswaga Bwana Choya Alex alisema kuwa kuna zoezi lililofanyika ni la kutambua kuna kaya ngapi  ndani ya hifadhi kutokana na maelekezo ya wizara na ilifanyika kama   kama sensa na si uthaminishaji ambao huusisha watu wa kada mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya Kondoa Sezaria Makota akitoa maelekezo ya kuondoka katika pori la hifadhi ya Swagaswaga wananchi wa mtaa wa Mongoroma.
Wananchi wa mtaa wa Serya wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makota (Hayupo pichani) katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya 
Mkuu wa Wilaya Sezaria Makota akisistiza jambo kwa wananchi katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...