WATANZANIA wameshauriwa kununua bidhaa kwenye maduka yanayotambulika na kuacha kuamini matapeli wanaotumia nembo za kampuni kubwa kuwahadaa.

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Kampuni ya Elite Computers yenye dhamana ya kusambaza bidhaa za Apple hapa nchini, wakati wa hafla ya kutambulisha simu mpya ya iPhone XR.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Aqil Kurji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Elite Computers alisema pamoja na kwamba Apple inaaminika kwa kuzalisha bidhaa bora lakini kumekuwa na wajanja wachache ambao wamekuwa wakitumia nembo ya kampuni hiyo kwa kuwauzia watanzania bidhaa zisizo na ubora.

“Leo Elite Computers ambao ni wakala rasmi wa Apple nchini tumetambulisha simu mpya ya iPhone XR  ambayo tunaamini kuwa itaendana na mazingira ya Kitanzania kwa asilimia 100 kutokana na kuzingatia hali halisi.

“Sifa kuu ya simu hii kwanza inadumu na chaji kwa saa 25 hadi 65 pia ina usalama kwani mteja atatumia uso wake kama paswedi(Face Id) na hivyo itarahisisha masuala ya wizi wa fedha kwenye simu jambo ambalo limekuwa likikemewa na serikali kwa muda mrefu hivyo iPhone XR ni ya kipekee ukilinganisha na matoleo yaliyopita.

“Kumekuwa na watu wengi wanaowadanganya watanzania kuwa ni mawakala wa Apple na badala yake wakiuziwa bidhaa hizo zisizo halisi wanakuja kulalamika kwetu jambo ambalo wanapaswa kuliepuka,” alisema Kurji.

Pia alifafanua kuwa mteja anaweza kupata matengenezo kwa kutembelea ofisi za Elite Computers zilizoko Upanga, Samora, Viva Towers, Seacriff village na Mwanza na kuongeza kuwa mteja anunuapo simu ghiyo atapata dhamana ya mwaka mmoja.

Upande wake Hussein Hassan ambaye ni mfanyabiashara wa simu nchini aliipongeza kampuni hiyo kwa kutamulisha simu hiyo ambayo alisema kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania kununua simu hiyo ili kuondokana na ununuaji wa simu zisizo na kiwango mara kwa mara.

“Hili ni jambo la kupongezwa kwa kampuni ya Apple kwani simu hii inausalama na kama tulivyoelezwa hapa kuwa ina uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa zaidi ya dakika 30 bila kuharibika hivyo ni jambo la kupongezwa kwani sisi wengi shughuli zetu zimekuwa ni za pilikapilika.

“Hivyo ni bora ukajinyima lakini ukamiliki simu yenye usalama na uhakika zaidi na pia inayodumu na chaji kuliko kuepuka gharama matokeo yake unakuwa wa kununua simu kila wakati,” alisema Hussein.

Mara kwa mara serikali imekuwa ikitilia mkazo kwa watanzania kuhakikisha kuwa wananunua bidhaa bora ikiwamo kudai risiti huku pia ikisisitiza kuongeza usalama kwenye simu zao ili kuzuia wizi wa fedha unaoweza kutokea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...