JUMLA ya wateja 100 wa Benki ya NMB wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine sita wakijishindia simu janja 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja. Idadi ya wateja hao imefikiwa leo baada ya kuchezeshwa droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata' na wateja wengine 20 kujipatia kitita hicho.

Droo ya tano imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam katika Tawi la NMB Oyster Plaza na kupatikana kwa washindi hao 20 chini ya uangalizi wa Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy.

Akizungumza katika droo hiyo Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala Alisema wateja 20 wamepigiwa simu na kujulishwa ushindi wao na fedha walizojishindia zitaingizwa kwenye akaunti zao ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo.Alisema kupatikana kwa washindi wa leo kunatimiza idadi ya wateja 100 hadi sasa ambao wamejishindia shilingi 100,000 kila mmoja, huku kukiwa na wengine 6 walionyakuwa simu aina ya Samsung S9+' droo iliyopita.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.

Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano zima.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Oyster Plaza, Hildegard Mng'ong'o akizungumza leo kwenye droo ya tano ya Masta Bata iliyochezeshwa katika tawi hilo. 


Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy na Florence Mchau kutoka kitengo cha kadi cha NMB (katikati). 

Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala (kulia) akizungumza leo kwenye droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto droo hiyo ikiendelea kuchezeshwa. 
Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy na Florence Mchau kutoka kitengo cha kadi cha NMB (katikati). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...