Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akifungua kikao kazi cha kuandaa jumbe za kuelimisha jamii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku na wa kwanza kushoto ni Bw. Christopher Mushi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanao kaa mjini singida kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Bw. Christopher Mushi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii akitoa mada kuhusu Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.



Na Anthony Ishengoma -Singida

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka watendaji wa serikali Mkoani Singida kuanzisha vituo vya Mkono kwa Mkono (One Stop Centres) ili waanga vitendo vya ukatili waweze kupata huduma kwa haraka tofauti na sasa wanapokumbana na mlolongo wa taratibu unaochangia kupotea kwa ushaidi.

Dkt. Lutambi amesama hayo leo mjini Singida wakati wa kikao chake na baadhi ya watendaji wa mkoa wake wanaotengeneza jumbe za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.

Aidha Dkt. Lutambi amewataka watendaji hao kutengeneza jumbe ambazo zitatoa elimu pamoja na mambo mengine itawawezesha waanga wa ukatili kupata mahali pa kukimbilia ndio maana amewaagiza kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono kwa lengo la kuwapatia huduma ya haraka waanga hao.

Aidha alitaja urasimu na taratibu ngumu zinazojitokeza baada ya muanga wa ukatili kufika katika vituo vya polisi ambapo waanga wanalazimika kufuata PF3 pamoja na kufuata milolongo ya kumuona daktari jumbo ambalo lianasababisha baadhi ya waanga kukata tamaa na wengine kurubuniwa na kubadili mawazo hivyo kuacha vitendo hivyo viendelee kutokea.

‘’Muhanga wa ukatili anapofika polisi anadaiwa PF3 akifika hospitali anakuta Daktari wa zamu hayupo na wakati mwingine akifika polisi anaambiwa polisi wako doria jambo linalotoa mwanya wa kushawishiwa na watendaji wasio kuwa waadilifu na hatimaye kubadili mawazo’’. Aliendelea kusema Dkt. Lutambi.

Aidha Dkt. Lutambi pia amewataka ndugu pamoja na raia wema kushirikiana na madawati ya jeshi la polisi kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili kwa kutoa ushaidi mahakamani kwani kesi nyingi mahakamani zinakwama kutokana na kukosa ushahidi.

Kwa mantiki hiyo basi mewataka watendaji hao kuweka mifumo imara itakayowezesha watendaji na waanga wa ukatili kufanikisha kukomesha vitendo vya ukatili sio tu kwa Mkoa wa Singida bali pia Tanzania nzima.

Wakati huo huo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku wakati akiongea na vyombo vya habari ameutaja Mkoa wa Singida kuwa ni miongoni mwa mikoa mitano Nchini Tanzania inayoongoza kwa ukeketaji.

Ameitaja mila ya ukeketaji kama mojawaopo ya mila inayopaswa kuachwa kwa kuwa inaacha makovu ya kisaikoloijia kwa mtu anayepata kufanyiwa tohara lakini pia ina madhara katika suala zima la Afya ya uzazi kwani mlengwa anaweza kupoteza maisha wakati wa kujifungua.

Aidha Mkurugenzi huyo amewataka wananchi mkoa wa Singida kubadilika kifikra na kuacha vitendo vya ukatili ambavyo kwa mazingira ya ulimwengu wa kisasa hayana na nafasi tena.

Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...