Na Samwel Mtuwa - Dodoma

Waziri wa madini Mh Doto Biteko leo  Januari 17/2019 amekutana na wawekezaji wa kiwanda cha Nyakato Gold Refinery (NGR) ofisini kwake jijini Dodoma , wenye nia ya kufungua kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu kwa kiwango cha asilimia 99.5 kwa lengo la kuongeza thamani pamoja na kuboresha soko la dhahabu nchini inayotoka kwa wachimbaji wadogo na wakati. 

Kabla ya majadiliano kuanza waziri Biteko alipokea taarifa juu ya namna ya kiwanda hicho cha NGR kitakavyofanya kazi ya ununuzi na usafishaji wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wakati, ambapo baadhi ya mapendekezo yaliyowasilishwa na NGR ni juu ya matarajio ya usafishaji wa dhahabu kwa kiasi cha kg50 kwa siku na tani 1.5 kwa mwezi. 

Baada ya majadiliano hayo waziri amewataka wawekezaji hao kuandaa na kuwasilisha andiko la mpango mkakati wa wazi utakaonesha namna uendeshaji wa kiwanda hicho utakavyofanyika ikiwa pamoja na namna serikali itakavyofaidika na uwekezaji huo ndani ya sekta ya madini. 

Tanzania ni nchi ya nne barani afrika katika uzalishaji wa madini ya dhahabu ikiongozwa na nchi ya Ghana naAfrika kusini . 

Pichani waziri wa madini Mh Doto Biteko mwenye suti ya rangi ya Blue aliyekaa mbele akiwa ofisini kwake jijini Dodoma akiongea na wawekezaji wenye nia ya kufungua kiwanda cha kusafisha dhahabu kitakachojulikana kwa jina la Nyakato Gold Refinery (NGR), wengine waliyekaa upande wa kushoto mwekezaji mwenye asili ya India Vaya Rajendra, anayefuata pembeni upande wa kulia ni Baraka Ezekiel yeye ni muhamasishaji kutoka NGR, wengine waliokaa upande wa kulia katika sofa ni watendaji kutoka wizara ya madini pamoja na Tume ya Madini wakifuatilia majadiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...