Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na baadhi ya Wanachama wa NSSF waliofika kwenye ofisi za NSSF Ilala/Temeke leo kufuatilia madai yao mbalimbali kufuatia maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii(SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam. Waziri Mhagama akiwa ameambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio amefanya ziara leo katika ofisi za Ilala,Temeke na Kinondoni kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Rais na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo Wanachama hao wakati wa kufuatilia madai yao kwenye ofisi hizo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio,wakati alipofanya ziara leo ya kutembelea ofisi za Ilala,Temeke na Kinondoni kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Rais na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanachama katika ofisi hizo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi wa NSSF wakimsikiliza mmoja wa Wanachama akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa kufuatilia madai yao ya mafao. 
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tusiime,Nobert Kamugisha ambaye amekwenda  kufuatiia madai yake kwenye Ofisi za NSSF Ilala Boma leo,akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo mbele ya  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Baadhi ya Wanachama wa NSSF wakiwa kwenye Ofisi za Ilala Boma wakifuatilia madai yao mbalimbali,walipokuwa wakimsikiliza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio akitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo madai ya Wanachama wa shirika hilo,mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama .

Baadhi ya Wanachama wa NSSF wakiwa kwenye Ofisi za Ilala Boma wakifuatilia madai yao mbalimbali,walipokuwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi wa NSSF wakiwasikiliza baadhi ya Wanachama wa shirika hilo waliofika kufuatilia madai yao mbalimbali katika ofisi za shirika hilo zilizopo Ubungo Plaza,jijini Dar.

======  ======  ========

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATOA MAAGIZO KWA NSSF, AKERWA NA TABIA YA NENDA RUDI KUFUATILIA MAFAO 

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge, Kazi ,Vijana na Ajira) Jenista Mhagama ameutaka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuhakikisha wanalipa mafao ya wastaafu kwa wakati huku akiwataka watumishi wa mfuko huo kufanya kazi kwa kujituma ya kuhudumia wastaafu nchini.

Mhagama ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ofisi za NSSF za Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia iwapo maagizo ya Rais Dk.John Magufuli ya kuwalipa wastaafu ambao wanadai mafao yao kama yameanza kutekelezwa ama la. Akiwa kwenye ofisi hizo Waziri Mhagama amesema, ameshuhudia maagizo ya Rais Magufuli yameanza kutekelezwa na NSSF lakini bado kuna baadhi ya changamoto ambazo lazima zipatiwe ufumbuzi. 


Amesema,moja ya changamoto ni tabia ya nenda rudi kwa wastaafu na wanapowaambia waondoke wanaondoka na fomu zao badala ya kuacha zishughulikiwe."Tabia hii ya nenda rudi sasa iwe basi na nimeshatoa maagizo ya kuwepo kwa mabango yenye namba za simu zote kwa kuwekwa wazi,"amesema.

"Waziri Magufuli amesisitiza umuhimu wa mafao ya wastaafu kushughulikiwa kwa wakati na kama watumishi hawatoshi kwenye ofisi hizo za Ilala na Temeke basi walioko makao makuu wahamishiwe kwenye ofisi hizo ili kutoa huduma kwa wanachama wao"."Ni vema NSSF wakahakikisha wanatoa huduma bora kwa wanachama, Kipaumbele lazima kiwe kuwahudumia wanachama wetu ambao ni wastaafu kwani wamefanya kazi kwa heshima, wao ni mashujaa na lazima washughulikiwe kishujaa badala ya kuwasumbua,"amesema Waziri Mhagama.

Amesema kuna baadhi ya watumishi wa NSSF wamekuwa na kauli za hovyo kwa wanachama wao na hivyo kutoa maagizo kwa kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kujituma kama sehemu ya kuenzi kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli ya kuwapigania wastaafu nchini.

Pia amesema kuna mameneja ambao wanataka kuonwa kwa apointiment na hivyo ametaka tabia hiyo iachwe mara moja na kwamba hata yeye ofisini kwake wanaohitaji kumuona wanakwenda bila apointment.Waziri Mhagama amewataka NSSF kufanya mabadiliko ya kimfumo ya kiutendaji kwa lengo la kuleta ufanisi wa kuwahudumia wanachama wao na kwamba anachotaka kuona ni kwamba kuna kuwa na urahisi wa kulipwa kwa mafao."Kuwe na malipo jana, yaani kwa maana ya kwamba wakati mwanachama anakuja NSSF tayari akute utaratibu wa kushughulikia malipo yake ulishafanyika kabla na anapokuja ni kuchukua fedha zake na kuondoka,"amefafanua Waziri Mhagama.

Wakati huo huo, Waziri Mhagama amesema kuna baadhi ya watu wasiowaaminifu wanatumia kipindi hiki kutaka kufanya udanganyifu ili walipwe mafao kwa kupeleka nyaraka za uongo na hivyo amewataka wenye
tabia hiyo watambue watachukuliwa hatua."Kuna baadhi ya watu wanakwenda na vielelezo feki ili wapewe mafao na NSSF, tutaanza kuja na askari kanzu kwa ajili ya kuwakamata watu wa aina hiyo ambao kimsingi wanataka kufanya utapeli.Pia kwa NSSF lazima mboreshe mfumo wenu ambao utabaini wale wanaotaka kufanya utapeli wa fedha hizi za wanachama,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Suala la mafao kwa wastaafu limekamilika, tuangalie suala la fao la kujitoa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. Imekuwa ni kero kwani vijana wengi wanamitaji lakini imeshikiliwa na NSSF. Sote ni ndugu, tulitazame upya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...