Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) alipokua anamfafanulia wakati walipokuwa wanaagana mara baada ya kumaliza kikao chao cha kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, wapili kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa UNHCR, Zephania Amuiri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, mara baada ya kumaliza kikao chao cha kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, na wapili kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa UNHCR, Zephania Amuiri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, na kujadiliana masuala mbalimbali ya wakimbizi nchini.

Waziri Lugola pamoja na Mwakilishi huyo, pia walijadiliana masuala ya ushirikiano kati ya Serikali na Shirika hilo la Kimataifa kwa mujibu wa sheria zinazowaongoza.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Jumapili, Lugola alisema Wizara yake haiwezi ikafanikiwa kikamilifu katika masuala ya kuwahudumia wakimbizi nchini kama haitashirikiana ipasavyo na UNHCR.

“Licha ya kuwa baadhi ya wakimbizi wanaendelea kurudishwa kwa hiari nchini kwao Burundi, lakini katika kufanikisha zoezi hili, lazima tushirikiane ipasavyo kati ya Serikali pamoja na nyie UNHCR, naamini Wizara yangu itafanya vikao nanyi mara kwa mara ili kufanikisha zoezi hilo pamoja na mengineo yanafanikiwa,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNHCR, Kapaya, alisema Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika lake vizuri, na jambo lolote la majadiliano linapotokea ujadiliana ili kuweka sawa ushirikiano huo. “Mheshimiwa Waziri mimi nakushukuru sana kwa kuniruhusu kuja kufanya mazungumza nawe, nimefarijika na haya madiliano na pia tutaendelea kushirikiana zaidi,” alisema Kapaya.

Katika kikao hicho Mwakilishi wa UNHCR aliambatana na Msaidizi wake Zephania Amuiri, na Waziri Lugola aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara yake, Harrison Mseke

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...