Watumishi wa Wizara ya Maji wamepanda miti katika eneo la Ihumwa kwenye mji wa serikali zoezi lililoongozwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa.
Jumla ya miti 600 imepandwa na watumishi wa Wizara pamoja na viongozi akiwemo Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo.
Profesa Mbarawa ameelekeza teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji itumike ili miti yote ilipandwa ikue. Amesema kuwa zipo teknolojia mbali mbali za umwagiliaji ambazo wataalamu wetu wanatakiwa kuzijua na kuzitumia.
Zoezi la upandaji miti kwenye kiwanja cha Wizara liliwahusisha wataalamu wa misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambayo imetoa miti hiyo ikiwa ni kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani.
Awali, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Kalobelo alisema kuwa, tayari Wizara ya Maji ina kisima kitakachotumika katikaumwagiliaji wa miti na bustani za wizara hivyo miti iliyopandwa itatunzwa kama inavyotakiwa.
Kwa mujibu wa TFS kwa jiji la Dodoma wastani wa asilimia 35 ya miti inayopandwa ndiyo hukua hivyo uangalizi wa karibu ni muhimu kuhakikisha miti yote iliyopandwa inakua. Jumla ya watumishi 300 walishiriki zoezi la upandaji miti katika mji wa Serikali - Ihumwa kwenye kiwanja cha Wizara.
 Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiotesha mti katika mji wa Serikali, eneo la Wizara ya Maji, Ihumwa jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akiotesha mti katika mji wa serikali, eneo la wizara yake, Ihumwa jijini Dodoma. Profesa Mkumbo amesema miti iliyooteshwa itatunzwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na tayari maji ya uhakika yapo.
 Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Emmanuel N.M Kalobelo akiotesha mti katika eneo la wizara yake, mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo (kulia) akikagua eneo la kuotesha miti, katika kiwanja cha Wizara ya Maji, mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kushoto, ni Mhandisi Tamin Katakweba, mmoja kati ya timu ya wizara iliyopo katika neno la ujenzi.
Viongozi wa Wizara ya Maji, kati, Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (Mb), kulia, Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo na kushoto Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Emmanuel N.M Kalobelo, pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maji baada ya kukamilisha kazi ya kuotesha miti 600, katika mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...