Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

YES We Can!Ndivyo unavyoweza kuuzungumzia ushindi wa timu ya Simba wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya JS Saoura katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Slaam.

Kabla ya mchezo huo uliofanyika jana jioni ya Januari 12,2019 ,Simba kupitia Msemaji wake Hajji Manara walizundua kampeni ya Yes we can ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili inasema Ndio Tunaweza kwa lengo la kuhakikisha wanashinda mchezo huo na ndicho kilichotokea.

Umahiri,umaridadi wa pasi, akili ya soka na kila aina ya udambwidambwi kwa wachezaji wa Simba ulitosha kuwafanya wachezaji wa timu ya JS Saoura kushindwa kumiliki vema mpira na hivyo wachezaji wa Simba kuonekana kuumiliki kila idara.

Dakika ya 45 mshambuliaji nyota wa Simba Emmanuel Okwi alipeleka shangwe,nderemo na vifijo kwa Simba na mashabiki wa soka nchini baada ya kupachika bao la kwanza.Uwanja mzima ulizizima kwa shangwe kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa Simba .Hivyo wakati wanakwenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja.

Katika mchezo huo wachezaji wa JS Saoura walionekana kutohimili stamina za wachezaji wa Simba kwani mara kwa mara walionekana wakianguka.
Kipindi cha pili cha mchezo huo kilianza kwa kasi huku kwa Simba wakiwa na hamu ya kutaka kuongeza mabao wakati JS Saoura nao wakionekana kutaka kusawazisha.

Hata hivyo kwa Simba ambao walioonekana kuendelea kulisakama lango la wapinzani wao. Kutokana na kusakata kabumbu vema Simba walifanikiwa kupata mabao mengine mawili kupitia kwa mchezaji wake Medie Kagere.
Hakika ushindi wa Simba uliwafanya mashabiki wa soka kuwa na furaha ambapo kila aliyeuzungumzia mchezo huo wameonesha kuwa na matumaini na timu hiyo kufanya vema kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Michuzi Blog ilipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe ambapo ameuzungumzia mchezo huo na kwamba ameridhishwa na kiwango cha Simba ambacho wamekionesha uwanjani hapo.

"Kwa leo mimi ni mshibaki wa Simba,na ikitokea kesho timu yetu nyingine ikacheza na timu ya nje ya Tanzania nitakuwa kwa timu ya nyumbani.Simba wamecheza vizuri sana leo," amesema Waziri Mwakyembe.

Alipoulizwa anatoa ujumbe gani kwa mashabiki wa soka nchini,Waziri Mwakyembe amejibu kuwa ni vema kuwa na uzalendo na timu za nyumbani zinapocheza na timu za nje."Tuwe wamoja timu zetu zinapocheza na timu kutoka nje.Ndio maana leo nilikuwa naishangilia Simba."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...