Msanii mahiri katika miondoko ya kughani a.ka Rap Golden Mbunda almaarufu kwa jina la Godzilla amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam alikopelekwa usiku wa kuamkia leo akiwa anasumbuliwa na presha na malaria.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa marehemu huko Salasala. Tutaendelea kuwajuza zaidi kadiri taarifa zaidi zitakavyotufikia.

Marehemu Godzilla alijizolea umaarufu kwa vibao vyake vingi kama vile "Nataka" na "King Zilla, na pia kwa uwezo wake mkubwa wa kughani papo kwa papo kwa njia ijulikanayo kama Freestyle.

MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI - AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...